0
Uhaba wa vifaa tiba na ubovu wa mashine za mionzi umewafanya wahudumu wa afya katika Taasisi ya Saratani Ocean Road kutibu wagonjwa hadi usiku wa manane .

Utafiti uliofanywa na Gazeti la MWANANCHI umebaini kuwa wauguzi hao wamejikuta wakitoa tiba kwa wagonjwa wa saratani hadi usiku kutokana na kuwepo kwa mashine moja baada ya ile nyingine kuharibika kwa kipindi cha miezi miwili sasa.

Kaimu Mkurugenzi wa Taasisi hiyo Diwani Msemo alisema hospitali hiyo ilikua na mashine mbili lakini kwa sasa imebaki moja na hulazimika kutoa huduma kwa kuangalia hali ya mgonjwa na kipaumbele kimetolewa kwa wagonjwa wa saratani ya kizazi na koo.

“Inatubidi kutoa kipaumbele kwa wagonjwa wenye saratani za koo kwa sababu wengi wao wanashindwa kumeza hata chakula au mate,pia wanawake wenye saratani ya kizazi nao wako kwenye hali mbaya,wengi wao wanatokwa damu mfululizo,”Alisema.
 Aidha alisema kwa kuwa magonjwa ya Saratani yanazidi kuongezeka kila siku,Serikali haina budi kuomba misaada kutoka kwa wahisani ili waweze kukabiliana nao kutokana na ukosefu mkubwa wa fedha walionao kwa sasa

Post a Comment

AddThis

 
Top