0

Ama kweli duniani kuna mengi,hii imetokea huko nchini Uganda baada ya mwanamke mmoja mwenye watoto watatu katika Wilaya ya Kole kumwandalia mumewe mlo wa mipira ya kiume ya kondomu kufuatia ugomvi usiokwisha baina yao.
Maamuzi ya mwanamama huyu  yanaweza kukushangaza sana kwani pamoja na familia za wanandoa wengi kuwa na kawaida ya kutofautiana wakati mwingine ni nadra sana kuona maamuzi yanayofanana na haya yakitolewa.
Kwa mujibu wa Gazeti la Daily Monitor  mwanamke huyo aliripotiwa kununua paketi tatu za kondomu aina ya Trust kutoka duka la jirani kabla ya kuzipika na kumwandalia mumewe kama chakula baada ya kurudi nyumbani akiwa amelewa chakari.
Baada ya kununua alirejea nyumbani na aliikatakata mipira hiyo  ambayo ilikua haijatumika katika vipande vidogo na kisha kuvichemsha kwa muda na baadaye kukaanga na mafuta pamoja na viungo vingine na kumpa mumewe ambaye licha ya ulevi wake alibaini  chakula kilikua na ladha tofauti.
Hata hivyo mwanamke huyo alisema alilenga kumfunza mumewe adabu kutokana na tabia yake hiyo inayomkera ya kurudi nyumbani akiwa amechelewa na amelewa sana.

Post a Comment

AddThis

 
Top