0
MUSOTI (KUSHOTI) WAKATI AKIITUMIKIA SIMBA. HAPA AKIWA MAZOEZINI NA SHABANI KISIGA KAMBINI ZANZIBAR.

Beki wa zamani wa Simba, Donald Musoti, ameendelea kuibana klabu hiyo katika kesi ya madai yake ya kuvunja mkataba kwa kusema kuwa Simba imeshindwa kuwasilisha vielelezo vya ushahidi katika Shirikisho la Soka la Kimataifa (Fifa).

Akizungumza kutoka Nairobi, Kenya, Musoti alisema Fifa wameamua kesi yake isikilizwe kuanzia wiki ijayo kwa upande mmoja kutokana na Simba kushindwa kuwasilisha vielelezo vyao kama walivyotakiwa.
“Mwanasheria wangu, Felix Majani, ameniambia kesi itasikilizwa kwa upande mmoja baada ya Simba kushindwa kuwasilisha vielelezo vyao kama walivyoombwa awali.
“Nadhani watakuwa wamekosa cha kupeleka kwa sababu hakuna kitu ambacho kinaweza kuwasaidia kujitoa katika kesi hii.
“Unajua sikutaka kesi yangu isikilizwe na TFF kwa sababu ni wazi nisingeweza kushinda kutokana na wao wangefanya ujanja-ujanja mwingi lakini Fifa hakuna kitu kama hicho, lazima haki yangu ipatikane,” alisema Musoti.

Simba ilivunja mkataba na beki huyo na nafasi yake kuchukuliwa na Emmanuel Okwi, kesi hiyo ilisimamishwa kusikilizwa baada ya Simba kuomba kupewa muda mpaka Oktoba 23, mwaka huu kuwasilisha vielelezo vyao vya kuvunjwa kwa mkataba huo.

Post a Comment

AddThis

 
Top