0
Mwanzo mzuri: Ilimchukua dakika saba tu Zlatan Ibrahimovic kufunga bao la kuongoza.
ZLATAN Ibrahimovic aliwaokoa mabingwa watetezi kupata kipigo katika mchezo wao wa ufunguzi wa ligi ya Ufaransa baada ya kufunga mara mbili katika sare ya 2-2 dhidi ya Stade de Reims jana usiku.

Nyota huyo alifunga bao la kuongoza katika dakika ya saba, lakini alikosa mkwaju wa penalti katika dakika ya 13.
Kiungo wa Reims,Prince Oniangue alisawazisha bao hilo katika dakika ya 22 kabla ya  Devaux kuwafungia wenyeji bao la kuongoza dakika 12 baadaye.
 Mwokozi wa PSG: Zlatan Ibrahimovic akishangilia bao lake na  Lucas Digne na Edinson Cavani   

Kiungo wa Reims  Antoine Devaux akipongezwa na wenzake baada ya kufunga goli.
PSG iliwakosa nyota wake Ezequiel Lavezzi, David Luiz, Maxwell, Blaise Matuidi na Yohan Cabaye, ambao wanaendela kujiimarisha baada ya kucheza fainali za kombe la dunia.
Beki wa Brazil, Luiz alinunuliwa kwa paundi milioni 50 mwezi juni mwaka huu akitokea Chelsea na kuweka rekodi ya kuwa beki ghali zaidi duniani. 


Post a Comment

AddThis

 
Top