MUZIKI NA MAADILI YA UMMA INCHINI CONGO DRC
KATIKA UCHAMBUZI WANGU HUU, NIMEWEKA VIDEO AMBAYO YAONYESHA UKEUKAJI WA MAADILI YA UMMA KUTOKANA NA MUZIKI. TIZAMA KWENYE VIDEO HII ANZIA DAKIKA YA ( 58:55 hadi 1:01:10 ). ASANTENI
Baadhi ya Wanamuziki Inchini CONGO DRC,katika Nyimbo zao hutumia Maneno Machafu,huku Wanenguaji wakicheza bila Aibu hadi wengine hufikia hatua ya kuvua kabisa Nguo zao na Kuonyesha sehemu zao za siri.
Ingawa Imefikia wakati fulani Serekali ya CONGO imechukua hatua ya kudhibiti vitendo vichafu kwenye Muziki,kupitia WIZARA YA UTAMADUNI NA SANAA, wakati lilipoundwa ” BODI YA MAMLAKA YA UDHIBITI WA MAMBO YAPOTOSHAO UMMA KWENYE MUZIKI “.
Licha ya kuwepo Shirika hilo, Bado wapo Wanamuziki ambao wanaendelea bila woga wowote kwenda kinyume cha sheria nakuyafanya hayo wayatakayo wao.
Kumbukeni zipo aina ya Dansi zilizo vuma sana wakati, Maneno yake yalikua ya Upotovu wa Jamii :
1. KOFFI OLOMIDE kaimba ( MAMAN PESA SIMA, PAPA ATUBA TONGA ) akimaanisha MAMA LETE NYUMA, BABA ACHOME SINDANO.
2. WERRASON ( yeye katuletea Dansi MFUENI = MATAKO, pia na DANSI MWANA NATIKAKA MOKE SIMA EKOLI akimaanisha KABINTI NILIKAACHA BADO KADOGO LEO HII KANAJAZA TAKO KAMA NINI ).
3.JB MPIANA nae hajabaki nyuma,na Dansi ( EZO SUA EZO SALA PASI, SIMBA NGA MALEMBE. akimaanisha YANICHOMA,YANIUMIZA KWELI,NENDA TARATIBU.
Mifano ni nyingi sana,ionyeshayo utovu wa nidhamu na Upotevu wa Maadili ya Umma kwenye Muziki. Hebu jifikirie wewe Mzazi na Watoto wako Sebuleni mkitizama Video iliojaa na Maneno machafu kama hayo,huoni kama ni Aibu tupu!!!
Licha ya Mimi Binafsi kua Mpenzi Mkubwa wa Rumba, Naona upo upungufu fulani kwenye Bodi ya Mamlaka ya kudhibiti mambo machafu kwenye Muziki.Haifanyi kazi yake ipasavyo kwakutoitekeleza majukumu yake vilivyo.
KATIKA DESTURI NA MILA ZETU KWA SISI WA AFRICA,MAMBO KAMA HAYO HUA HATUPENDEZWI NAYO HATA KIDOGO.
Mambo kama hayo, na Vitendo kama vivyo, ni Moja ya sababu iliopelekea Vijana wa Diaspora wa CONGO, wanao julikana kwa jina la ” COMBATTANTS ” kuja juu na kupinga vikali aina ya Muziki kama huo, kwa madai kwamba SIKU HIZI MUZIKI WATUMIWA VIBAYA KWA KUPOTOSHA JAMII NA KUMDHALILISHA MWANAMKE.
Kwenye Miaka Kadhaa iliopita,Ilikua vigumu kwa Mwanamuziki kuimba maneno machafu,pasipokua na Sheria kufanya kazi yake. Kumbukendi kipindi ambacho Sheria kali imechukuliwa Dhidi ya Wanamuziki KOFFI OLOMIDE na NYOKA LONGO,walipo swekwa jela Mwaka 1993 JIJINI KINSHASA, kutokana na Dansi ” ETUTANA EH YANGO NA YANGO ” VIACHENI VIGONGANE VYENYEWE KWA VYENYEWE.
Sasa ingawa siku za huko Nyuma,Sheria ilikua ikifanya kazi na kuwapa adhabu kali kwa wale ambao wanaharibu maadili ya Umma kupitia Nyimbo zao, Kwa nini leo hii Wanamuziki wanaipa sheria kisogo, na kufanya yale wayatakayo bila kua na woga wowote?
Je! Hali hii ya sababishwa na Viongozi wenyewe wa Serekali,ambao hujisahau kutokana na Maslahi yao binafsi,kwakua kupitia Wanamuziki hujipa umaarufu zaidi wanapo tajwa mara kwa mara kwenye NYIMBO ?( LIBANGA ).
WENGI TULISHEHEREKEA KUONA SEREKALI YA CONGO IMEWATUNZA WANAMUZIKI KWA KUWAPA TUZO KUTOKANA NA KAZI YAO, NI WAJIBU PIA WA SEREKALI HIYO KUSISITIZA NA KUSHIKIZA MASWALA YA MAADILI MEMA KWA WANAMUZIKI,KWAKUA WAO NDIO KIOO CHA JAMI
Post a Comment