Didier Drogba ambaye amejiunga tena na club Chelsea baada ya kuondoka kwenye club hiyo kipindi kilichopita ameingia kwenye headline na story mpya. Drogba amekuwa captain ya timu ya taifa ya Ivory Coast kwa miaka 8 na kucheza kama mchezaji kwa miaka 12.
Hivi sasa ametangaza kustaafu kuchezea soka timu ya taifa. Didier akitangaza uamuzi huo alisema, “Ni masikitiko sana kwa kuamua kustaafu kucheza soka na timu ya taifa. Miaka 12 iliyopita nikiwa kwenye timu ya taifa, timu yetu ilikuwa na msisimko mkubwa.
Kuanzia mara yangu ya kwanza nilivyoitwa kucheza timu ya taifa hadi mechi yangu ya mwisho siku zote nilijaribu kutoa kilicho bora kwa ajili ya nchi yangu. Najivunia nilikuwa captain kwa miaka 8 na kuchangia kuiweka nchi yangu kwenye kiwango cha dunia kwenye soka.”
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Post a Comment