0

Mtu mmoja ‘ mbishi na asiyeshaurika’ anafanya anachotaka katika usajili wa Simba SC ambao unaendelea kipindi hiki cha usajili. Saady Kipanga, ni mchezaji wa nafasi ya kiungo wa mashambulizi ambaye pia ana uwezo wa kucheza katika nafasi ya ushambuliaji. Elius Maguli amesaini ili kuziba nafasi ya Edward Christopher ambaye ameachwa.

 Ujio wa mshambuliaji wa kimataifa wa Kenya, Paul Kiongera ni wazi kutachochea hamasa na mwamko zaidi kwa mshambulizi, Amis Tambwe ambaye alitwaa tuzo ya ufungaji bora msimu uliopita baada ya kufunga mabao 19 katika michezo 23 ya ligi kuu.

 Maguli alifunga mabao 10 kwa msimu mzima akiwa na klabu ya Ruvu Shooting, mabao tisa aliyafunga katika michezo 12 ya mzunguko wa kwanza kiasi cha kumshawishi aliyekuwa Mwalimu wa timu ya Taifa, Kim Poulsen kumjumuisha katika kikosi cha wachezaji 20 ambao waliiwakilisha Tanzania Bara katika michuano ya Mataifa ukanda wa CECAFA, Challenge Cup nchini Kenya mwishoni mwa mwaka uliopita. Mchezaji huyo tayari ametangazwa rasmi na makamu wa rais wa timu hiyo Geofrey Nyange Kaburu.

 Ni usajili mzuri ambao unaweza kumaliza tatizo la ukosefu wa magoli ambao wachezaji kama, Haruna Chanongo, Zahoro Pazzi, Betram Mwombeki, Ramadhani Singano walizipoteza kwa wingi msimu uliopita na kupelekea timu hiyo kufanya vibaya hata katika michezo dhidi ya timu dhaifu kama, Mtibwa Sugar, JKT Mgambo, Tanzania Prisons, JKT Ruvu, Ruvu Shooting. Je, kulikuwa na sababu yoyote ya Simba kumsaini, Kipanga?.

Geofrey Nyange ‘Kaburu’
Mpira wetu hauna kuheshimiana. Kiongera ni mshambuliaji, Tambwe ni mfungaji, Maguli ni mfungaji chipukizi mwenye kipaji kikubwa, je, hawa wanatosha kuifanya Simba SC kuwa na safu kali ya mashambulizi msimu ujao?. 

Achana na yote yanayozungumzwa kuwa mchezaji huyo wa zamani wa Rhino Rangers na Mbeya City amesajiliwa kutokana na shinikizo la makamu mwenyekiti wa klabu hiyo, Geofrey Nyange Kaburu, lakini kwa mtazamo wa kweli mwalimu, Logarusic alimuhitaji mchezaji huyo hata kabla ya Kaburu kuingia madarakani.

 Ndiyo, Kaburu ni mmoja wa viongozi wa soka nchini ambao wamekuwa wakiingilia majukumu ya mwalimu iwe katika usajili au upangaji wa timu. Milovan Curkovic amewahi kuelezea tabia ya kiungo huyo ambaye alimshinikiza kumpanga Singano katika mchezo wa ugenini dhidi ya Kiyovu ya Rwanda, Februari, 2012 katika mchezo wa kombe la Shirikisho barani Ulaya.


Kocha mkuu wa Simba sc, Zdravko Logarusic
Mwenyekiti wa kamati ya usajili ya klabu yupo bize kuhakikisha anafanikisha usajili wa wachezaji wa kulipwa kutoka nje ya nchi. Kama, Zacharia Hans Poppe anafanya kazi yake huku akiongozwa na mahitaji ya benchi la ufundi sioni tofauti zozote ambazo zimekuwa zikiripotiwa katika vyombo vya hali. Sioni tatizo kwa Kaburu kuishinikiza kamati ya usajili kumsaini, Kipanga kwa kuwa ni mapendezekezo ya muda mrefu kutoka kwa Mwalimu. Logarusic pia anamuhitaji,

 Kiongera mchezaji ambaye amemshuhudia wakati akifanya kazi katika klabu ya Gor Mahia ya Kenya kwa muda wa miaka miwili. 
Kipi kinachofanya vyombo vya habari kueneza taarifa kwamba hakuna maelewano kuhusu usajili wa Kipanga?. 
Bila shaka ni tabia ya makamu huyo mwenyekiti kushiriki katika kila maamuzi. Iwe ni kwa uzuri au kwa ubaya, Kaburu anatakiwa kuhepuka kuweka wazi kila kitu kinachopita mbele yake. Kama viongozi wote watafuata maelekezo ya benchi la ufundi, Simba itasajiliwa vizuri na lolote litakalotokea mtu wa kwanza kuulizwa atakuwa ni kocha.

  Kama sasa, Logarusic anashindwa kuheshiwa itakuwaje wakati msimu umechanga na timu haendi sawa uwanjani. Rahisi tu atajitetea kuwa amesajiliwa wachezaji na uongozi na kulazimishwa kuwatumia. Simba hawapaswi tena kujichanganya katika usajili wa safari hii kama kweli wanataka kuinuka katika soka la Tanzania.

 Muhimu wachezaji wasajiliwe kutokana na mapendekezo ya Mwalimu, na viongozi waheshimiane katika majukumu yao. Kila mmoja awajibike ipasavyo katika nafasi yake. 

Kitendo cha timu hiyo kuhamishia mazoezi yake katika uwanja wa Bunju ni kielelezo tosha kuwa hatua fulani inapigwa katika utawala, iwe hivyo pia kwa upande wa ndani ya uwanja. Benchi la ufundi liwe huru kufanya kazi yake. Baada ya Manyika Peter Manyika, Hussein Shariff, Mohammed Hussein, Maguli, Simba SC iendeleee kumsikiliza Mwalimu Logarusic katika mahitaji yake ya wachezaji. Hata mimi ningemsaini Kipanga kwa sababu ni mchezaji anayetakiwa na Mwalimu.

 Kamati ya usajili haitakiwi kupishana na mawazo ya Mwalimu na inapotokea hivyo sababu za msingi ziwepo na si mtu kufanya kazi kwa mtazamo wake pekee. 

Utawala wa juu kama unatambua uwepo wa kamati yao ya usajili, wanatakiwa kutoa ushauri tu lakini wanaweza kushinikiza jambo ambalo Mwalimu analihitaji hata kama kamati ya usajili inalikataa. Simba SC imetafunwa sana na usajili wa ‘ fulani’ ila imewahi kunufaika na usajili wa bechi la ufundi. Kila kitu hakiwezi kwenda sawa lakini hakuna sababu yoyote ya msingi kuwepo na mvutano katika usajili wa Simba.


Post a Comment

AddThis

 
Top