0

INGAWA UHUSIANO WA KIDIPLOMASIA WAINGIA DOSARI KATI YA NCHI ZA CONGO BRAZZAVILLE NA CONGO KINSHASA, KWANZA NI KITENDO CHA NCHI YA CONGO BRAZZAVILLE  KUWASAKA NA KUWATIMUA KWA NGUVU WA HAMIAJI HARAMU NCHINI HUMO,AMBAO WENGI WAO NI RAIA KUTOKA CONGO DRC, PILI NI KUTOKANA NA PENDEKEZO LA RAIS WA CONGO BRAZZAVILLE ” DENIS SASSOU NGUESSO ” LAKUTAKA NCHI YA CONGO DRC IRUDIE JINA LAKE LA ZAMANI LA ” ZAIRE “.


NA PAPO HAPO RAIS WA CONGO KINSHASA ” JOSEPH KABILA ” KAMJIBU KWA KUMDHIHAKI KANA KWAMBA ” NCHI YA CONGO BRAZZAVILLE INGELISTAHILI KUA MMOJA KATI YA MIKOA YA CONGO KINSHASA, NA RAIS DENIS SASSOU NGWESSO ANGETEULIWA MKUU WA MKOA HUO.

LICHA YA MALUMBANO HAYO,KOFFI OLOMIDE, KAALIKWA KAMA MGENI RASMI NA RAIS DENIS SASSOU NGUESSO  KWENYE SIKUKUU YA KUSHEHEREKEA UHURU WA INCHI YA CONGO BRAZZAVILLE, SHEREHE ILIOFANYIKA  KWENYE MJI WA ” SIBITI ” TAREHE 15-08-2014.

WAKATI AKIWA JUKWAANI, KOFFI OLOMIDE KASEMA ” INGAWA YEYE NI RAIA WA INCHI YA ZAIRE, ILA KAJIVUNIA MAENDELEO AMBAYO KAYAONA  INCHINI  CONGO BRAZZAVILLE.

KASEMA KWAKE YEYE RAIS WA CONGO BRAZZAVILLE, NDIE MZURI WA USO NA UMBO KUWAZIDI MA RAIS WOTE BARANI AFRICA.

KOFFI OLOMIDE KAIMBA WIMBO ” N’GOULI ” UNAO PATIKANA KWENYE ALBUM ” MONDE ARABE “, WIMBO HUO AMBAO NI UTUNZI MAALUM KWA AJILI YA MAMA “ANTOINETTE SASSOU NGUESSO ” YEYE AMBAE WAPINZI WAKE HUMPACHIKA JINA LA ” N’GOULI “, LIKIMAANISHA ” MAMA “.

MAMA ANTOINETTE NA MMEWE RAIS WALISHINDWA KABISA KUJIZUIA, WALISIMAMA NA KWENDA KULISAKATA RUMBA ” TCHATCHO “.HUKU WAKIFWATIWA NA UMATI WAWAALIKWA.

UTAMSIKIA KOFFI OLOMIDE AKIIMBA KWENYE WIMBO HUO  ” MAMAN N’GOULI NA PAPA NGUESSO NZAMBE ABATELA BINO EBELE ” / MAMA NA BABA NGUESSO ,MWENYEZI MUNGU AWAZIDISHIE NYINGI ZAIDI.

Post a Comment

AddThis

 
Top