KOCHA wa Chelsea, Jose Mourinho amegoma kusema kama bado anahitaji wachezaji wengine Stamford Bridge majira haya ya kiangazi.
The Blues wamewasajili Filipe Luis, Diego Costa, Cesc Fabregas na Didier Drogba kwa dau la jumla la paundi milioni 75 na Thibaut Courtois amerejea klabuni baada ya kumaliza mkataba wake wa mkopo katika klabu ya Atletico Madrid.
Mourinho licha ya kudai kuwa ana furaha na kikosi chake, amemuambia Petr Cech kuwa yupo huru kuondoka.
Hata hivyo, kocha huyo amesema bado anaweza kufanya usajili katika dirisha hili la majira ya kiangazi kwasababu muda bado upon a itategemeana na hali halisi.
Aliwaambia waandishi wa habari; “Soko bado lipo wazi na uzoefu unatuonesha kuwa wakati soko lipo wazi huwezi kusema kitakachotokea. Kama unajua wachezaji wako walikuwa katika kiwango fulani mara ya mwisho mwezi uliopita, hatuwezi kujua timu nyingine zinahitaji kufanya kitu gani kwa wachezaji wetu”.
“Lakini ukweli ni kwamba nina furaha na kikosi changu. Nina furaha na timu yangu na mfumo unaniunga mkono”
Inafahamika kuwa Chelsea imetuma maombi ya kumsajili mshambuliaji wa QPR, Loic Remy baada ya Didier Drogba kupata majeruhi ya kifundo cha mguu.
Pia dili la kumsajili mlinda mlango kinda Ivan Brkic linaelekea kukamilika.
Mourinho alieleza kuwa amevutiwa na wachezaji alionao katika kikosi chake na amekiri kuwa timu yake itakuwa katika mbio za ubingwa msimu wa 2014/2015.
“Tumeleta baadhi ya wachezaji muhimu tuliowahitaji katika kikosi chetu. Wachezaji hawa wametufikisha sehemu nyingine”.
“Ndio, sisi ni washindani wa ubingwa. Kama unanitaka nisema kama tutashinda ubingwa, siwezi, kwasababu ninaheshimu ushindani huu”.
Chelsea itaanza mbio za ubingwa dhidi ya Burnley katika dimba la Turf Moor siku ya jumatatu.
Post a Comment