Sasa hivi kutokana na hali ya hewa watu wengi wanaugua mafua na kikohozi.Mimi jana nilikuwa na hali mbaya kabisaa tena na homa juu nikajaribu kuomba ushauri kwa followers wangu katika ac yangu ya instagram.Nilielezwa mambo mengi ya kufanya ili kujipa unafuu wa mafua na kikohozi.
Pole mwaya kwa mafua mamii
One way ya kuzuia virus isisambae ni kutumia vitunguu maji kata katikati halafu weka Diferent areas kama jikoni, chumbani kwako, hata sebuleni if u dn mind.kikinyauka unabadil mpka mafua yatakapoisha.
Kitunguu maji hufyonza virus wote na hivo kupunguza kasi ya maambukizi ya mafua makali kwa wengine,ndo maana its advised kutokula kachumbari ya vituungu vibichi iliokaa muda bz it absorbs most of the virus
Kwa wewe kuzibua pua natural remedy fanya hivi
Tangawizi osha na maganda yake vipande vikubwakubwa ili (iweconcetrated) twanga,changanya na malimao yaluyokatwa vipande dumbukiza kwa sufuria ongeza vikombe viwili vya maji.chemsha kama dk 10 ongezea vitungu swaum vilivopondwa.chuja unakua unakunywa kidogokidogo mpka jioni u will feel good. Kila ukinywa shushia kijiko cha asali
Get wel soon mwaya
Kwa kuongezea tips zingine nilizopata na kuzifanyia kazi ni pamoja na kula machungwa kwa wingi machungwa yapo kama upo kwenye haka kaugonjwa jitahidi kula.Kama sikula machungwa basi kamua juisi yake.Pia ukiwa nyumbani badala ya kutembea peku kukanyaga chini vaa socks.Kunywa maji mengi Yasiwe ya baridi.Ukilala hakikisha unalalia mashuka masafi na usirudie shuka kulalia bila kuyafua pamoja na foronya za mito.Pia wakati wa kuoga jitahidi kuoga maji ya moto utajisikia vizuri na unafuu.
Kama kuna zingine naomba uongezee hapa tusaidiane.Kama ni dawa za hospital basi fuata ushauri wa daktari.
Home
»
» Unlabelled
» UNAPOKUWA NA MAFUA NA KIKOHOZI UNAJITIBU VIPI KWA KUTUMIA VITU VILIVYOPO NYUMBANI?
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Post a Comment