0


Mbarouk mwenye asili ya Zanzibar, ameiambia Goal ameichezea kwa kipindi cha misimu tisa timu hiyo ya Coventry City

KOCHA wa Yanga Marcio Maximo jana  amemkaribisha mshambuliaji wa  Coventry City  inayoshiriki ligi daraja la kwanza chini Uingereza Selemani Abdallah Mbarouk, kufanya mazoezi  na timu hiyo na endapo atamvutia aweze kumsajili kwa ajili ya kukitumikia kikosi chake msimu unaokuja
Mbarouk mwenye asili ya Zanzibar, ameiambia Goal ameichezea kwa kipindi cha misimu tisa timu hiyo ya Coventry City,na kupata uzoefu wa kutosha kuweza kuitumikia Yanga endapo Maximo ataridhishwa na kiwango chake.
“Wakala wangu Salimu ambaye nimekuwa naye tangu nipo kituo cha kukuza vipaji cha Afri Soccer cha Zanzibar ndiyo amenileta hapa Yanga ameniambia ni timu nzuri ambayo inaweza kunifikisha kule ambapo ninapataka”alisema Mbarouk.
Mbarouk aliyewahi kupitia Academy ya Chalsea ya Uingereza akiwa na miaka saba alisema alisifu mazoezi ya Maximo na uwezo wa wachezaji wa Yanga na kusema anahitaji kujifua zaidi ili aweze kuendana na kasi yao.

Chanzo: Goal.com
 


Post a Comment

AddThis

 
Top