0
Iko wapi ratiba ya ligi kuu ya soka Tanzania Bara, Vodacom Primier League msimu wa 2014/ 15?. 
Tanzania inataka kupiga hatua mbele kuelekea spka la kulipwa,klabu zimekuwa zikitumia kiasi kikubwa cha pesa ili kumarisha timu zao.

Hivi sasa kuna wachezaji ambao wanalipwa hadi milioni nne na kuendelea katika baadhi ya timu. Makocha bora kutoka nje ya nchi wanakuja kufanya kazi Tanzania huku wakilipwa vitita  vikubwa vya pesa. Je, sababu kama hizo zinaweza kuhalalisha usemi kuwa ‘soka la Tanzania lipo katika utaratibu mzuri wa soka la kulipwa?’.

Yanga SC, ipende timu hii,ila pia unaruhusiwa kuichukia kama wewe si mshabiki wake. Inategemea na upande ambao utaangukia katika ushabiki wako katika mpira wa Tanzania, lakini hii nitimu inayogusa maisha ya watu wengi katika nchi hii. 

Yanga ni mabingwa mara 24 wa Tanzania Bara ( mabingwa mara nyingi zaidi), Ndiyo timu ya kwanza kuanzishwa nchini Tanzania ( ilianzishwa mwaka 1935). 

Ndani ya uwanja ni timu iliyofanikiwa zaidi kuliko timu zote nchini. Yanga ni timu yenye mashabiki wengi zaidi nchini . Utambulishe mkuu wa Yanga ni rangi zake. Nyeusi, Njano na Kijani, basi.

Yanga ipo katika daraja la juu zaidi kwa miaka mingi. Hii ni ‘ timu ya wanachi’ kwa maana nyingine ni timu inayokubalika na kupendwa sana nchini. Katika maisha tunayoishi unaweza kujua ukweli wa haya niyesamayo. 

Yanga itaiwakilisha Tanzania Bara katika michuano ya kombe la klabu bingwa kwa ukanda wan chi za Afrika Mashariki na Kati, Kagame Cup nchini Rwanda kuanzia mwanzoni mwa Mwezi ujao wa Agosti. Yanga ni mabingwamara tano wa michuano hiyo ( wakilingana na timu za Tusker FC, AFC Leopards) huku timu inayoongoza kwa kutwaa ubingwa huo ikiwa ni mahasimu wao Simba SC. 

Tusker, Leopards,na Simna hazipo katika michuano ya mwaka huu hivyo Yanga inaingia katika michuano ikiwa timu bora kuliko zote. Naweza kusema ndiyo timu pekee ya michuano.
Rekodi ya Yanga katika michuano hiyo ni mikubwa, imetwaa mara tatu ubingwa huo michuano ikichezwa nje ya Tanzania, na imetwaa mara mbili mfululizo katika kipindi cha miaka mitatu iliyopita, Jijini, Dar Es Salaam. 

Sasa mabingwa hao ,mara tano wa kihistoria wanakwenda Rwanda wakiwa na kikosi kilichoshiba, huku wachezaji watano wa kimataifa wakitarajiwa kuanza katika kikosi cha kwanza. 
Yanga imepangwa katika kundi la Kwanza pamoja na timu za Coffee ya Ethiopia, Atlabara ya Sudan Kusini, wawakilishi wa Tanzania Visiwani, KMKM,na moja kati ya timu tatu wenyeji wa michuano, Rayon Sports.

Uhasama wa Yanga na Coffee ni wa muda mrefu tangu ‘ wababe’ hao wa soka la Tanzania walipoicha Coffee mabao 6-2 katika mchezo wa marejeano na kufuzu kwa hatua ya nane bora ya ligi ya mabingwa barani Afrika, mwaka 1998.

KMKM na Atlabara wanatarajiwa kuwa vibonde katika kundi hilo. Coffee ni mabingwa mara mbili wa michuano huku, Rayon ni moja ya timu ‘ kabambe’ katika ukanda wa CECAFA, na kitendo cha mabingwa hao wa Rwanda kupangwa pamoja na Yanga ni sawa na kukumbushia mipambano yao ya miaka ya nyuma katika michuano hiyo. Rayon dhidi ya Yanga ni moja ya mechi kubwa za soka katika ukandaa huu ila Yanga wamefanikiwa kuwa mbele ya timu hiyo hata wanapokutana.

MAKIPA WATATU BORA…..
Kocha, Mbrazil, Marcio Maximo, ambaye anasaidiwa na Leonardo Leiva na Salvatory Edward atakuwa na kazi ya kupanga timu yake katika usawa huku akiunganisha vipaji ‘ lukuki’ vilivyopo katika timu hiyo. Maximo ambaye asalipwa mshahara unaokadiliwa kufikia milioni 22 za Kitanzania, amefanya kazi na walinda mlango wote watatu ambao kimsingi wanaweza kumsaidia kufukia malengo yake. Juma Kaseja, Deo Munish ‘ Dida’ na Ally Mustapha wote hao wamewahi kufanya kazi na Maximo wakati akiwa kocha wa timu ya Taifa ya Tanzania kwa kipindi cha miaka minne.

Ujio wa Mwalimu huyo ni sawa na kufufua upya hali ya kujiamini kwa Mustapha ambaye hajapangwa katika mchezo wowote tangu alipofanya makosa katika mchezo wa ligi kuu kati ya Yanga na Simba uliomalizika kwa sare ya mabao 3-3. Licha ya kukiri kuwa na tofauti na Kaseja mara baada ya kusaini mkataba wa miaka miwili wa kuinoa Yanga, Maximo aliweka wazi kuwa kila kitu kimekwisha na sasa wapo katika upande mwingine wa mahusiano.

 Juma Pondamali ‘ golikipa wa zamani wa Afrika’ na timu ya Taifa ya Tanzania ndiye kocha wa makipa katika kikosi hicho cha Maximo kwa maana hiyo Yanga ni timu iliyokamilika katika idara ya ufundi. Dida ndiye kipa namba moja wa Taifa Stars, ila atakaporudi klabuni itambidi kupambana hasa ili kuwa kipa chaguo la kwanza. Kama ningekuwa katika nafasi ya Maximo ningewachesha wote hao kwa kupokezana, ila kisoka si vizuri kwa maana hiyi ni lazima timu iwe na kipa namba moja wa kudumu huku wasaidizi wake wakiwa tayari kubeba majukumu muda wowote watakaohitajika.

Unaweza kuipanga Yanga kiurahisi tu katika idara ya ulinzi kwa sababu wachezaji wanne wa nyuma ndiyo wanaounda ukuta wa timu ya Taifa. Oscar Joshua katika nafasi ya ulinzi wa kushoto, Kelvin Yondan na nahodha Nadir Haroub hawa wote wanaingia moja kwa moja katika kikosi cha kwanza cha Maximo, huku mchezaji wa kigeni,Mbuyu Twite akirudishwa katika nafasi ya mlinzi wa kulia. Maximo hataumiza sana kichwa kupanga wachezaji wanne wa idara ya ulinzi, ila wakati akitafari kuhusu chaguo la golikipa, nafasi ya kiungo ni ‘ pasua kichwa’.
NIYONZIMA, OMEGA NI SAFU SAHIHI YA KIUNGO
 
Kombe la Kagame itakuwa ni michuano ya Haruna Niyonzima?. Haruna alikuwa na kipindi kigumu sana kuanzia mwanzoni mwa mwaka huu, alipatwa na matatizo makubwa ya nje ya uwanja ambayo ilikuwa ni kitendo cha nyumba yake kuungua kwa moto. Aliporejea uwanjani hakuwsa Yule ambaye anauwezo wa kutembea na mipira katikati ya uwanja huku akigawa pasi sahihi kwa wachezaji wenzake, katika mzunguko wa pili wa ligi kuu Niyonzima alionyesha kiwango cha chini kiasi cha kuingia katika migogoro ya mara kwa mara na Mwalimu aliyepita, Hans  Van Der Plujm, chini ya Maximo ameonekana kumirika katika mazoezi ya timu hiyo, bila shaka arudishwa katika nafasi yake ya kiungo wa kati ili kufanya timu ijiamini uwanjani.

Usajili wa Omega Seme ni kama nyongeza katika nafasi ya kiungo, ila itakuwa si jambo zuri kumuacha nje mchezaji huyo ambaye amepandisha kiwamgo chake kwa kiasi kikubwa. Wakati Niyonzima ni kiungo aliyekamilika katika suala la kumiliki mpira, kupiga pasi za mwisho na kutawanya mipira, Omega ni mchezaji mwenye uwezo mkubwa wa kupiga pasi za umbali mrefu ambazo mara nyingi hufika kwa walengwa,ni mkabaji mzuri na mchezaji mwenye nguvu. Niyonzima anaweza kutrawala vizuri nafasi ya kungo kama atapangwa na mchezaji kama Omega ambaye licha ya kucheza tofauti na Athumani Iddi,mchezaji huyo ana uwezo wa kuendesha timu uwanjani na mtu anayejiamini muda wote.

Mrisho Ngassa, Saimon Msuva, hawa watapambana kuwania nafasi moja na mshindi katika vita hiyo anaweza kufiti kwa namna yoyote katika mbinu za Maximo. Wote wawili, Ngassa na Msuva ni wachezaji ambao wanapenda kumbia uwanjani. Ngassa ana uwezo wa kukimbia na mpira pia ana uwezo wa kukimbia katika nafasi, ni mchezaji wa hatari anapokuwa katika kiwango chake cha juu. Ila linapokuja suala la winga namba saba,Msuva ni mchezaji bora zaidi ya Ngassa kwa wakati huu. Kama Maximo atamuanmini,Yanga watandelea kunufaika na mfungaji huyo wa bao la mwisho katika ligi kuu msimu uliopita kws upande wao hakika watapata mabao ya kutosha.

NI JAJA NA OKWI,  TEGETE NA BAHANUZI+JAVU

Maximo ana wachezaji wa kutosha katika nafasi ya ushambuliaji. Machaguo ya Ngassa, Nizar Khalfan, Andry Coutinho inaweza kuwa nyongeza nyingine katika safu ya ushambuliaji wa kati na hata kurahisisha ubadilikaji wa mfumo wa kiuchezaji. Si ki-lugha tu, Yanga itabadilika kimfumo na kimpira kama wachezaji watamudu walau kucheza kwa nguvu kwa walau asilimia 50 ya uwezo wao.
 Kiasili, Yanga hupendelea kucheza mfumo wa 4-4-2 ambao hata kiungo wa kulia, Msuva amewahi kuniambia ndiyo mfumo unaopendwa na wachezaji wengi wa Kitanzania. Uwepo wa Mbuyu kama mlinzi wa kulia ama Juma Abdul, huku Ngassa au Msuva katika winga ya kulia ni wazi upande huo unaweza kuwa chachu ya mabao mengi ya Yanga. Maximo amemsaini, Jaja huku akisema kuwa mshambulizi huyo raia wa Brazil ni mpigaji mzuri wa mipira ya kichwa. Hatujamuona Jaja katika mechi ila hadi anakuja kufanya kazi Tanzania atakuwa mtu anayejua anachofanya. Msimu uliopita Yanga ilikuwa ikipoteza nafasi nyingi za kufunga lakini ndiyo timu iliyomaliza ligi ikiwa na mabao mengi zaidi, 61.

 Krosi nyingi zilipigwa kutoka upande wa kulia, iwe ni kutoka kwa Mbuyu, Abdul, Msuva au Ngassa mipira mingi ya krosi ilipotea. Jerry Tegete alifunga mabao machache akiunganisha krosi ila alipoteza nafasi nyingi zilizotengenezwa kwa mipira ya krosi. Ujio wa Jaja wala siwezi kuubeza, kuna asilimia fulani naamini utakuwa na faida kubwa. Michuano ya Kagame inaweza kutoa tafsiri kuhusu uamuzi wa Maximo kumtema Hamis Kizza na kumsaini Jaja.
 Ukiachana na ushabiki na kurudi katika uhalisia mshambulizi wa Simba SC, Amis Tambwe ni mfungaji makini na mchezaji anayejua kujipanga katika maeneo yake ya hatari, laiti kama angecheza katika timu ya Yanga msimu uliopita angefunga mabao mengi zaidi ya 19 aliyofunga katika kikosi kilichokuwa na hali mbaya katika ligi kuu msimu uliopita.

 Bahanuzi ni mchezaji ambaye anapojenga hali ya kujiamini analeta machaguo mengi katika uchezaji wa timu. Nafikiri ndiye mshambuliaji-mfungaji mwenye uwezo wa kucheza mfumo wowote ule. Anakontroo, mshambuliaji huru, ana uwezo wa kulazimisha mabeki kufanya makosa na kuwapita, ana uwezo wa kucheza kama mshambulizi pekee na kufunga mabao, anakimbia vizuri katika eneo la hatari la timu pinzani, ni mchezaji msumbufu kwa mabeki kutokana na kuhamahama kwake uwanjani hivyo kutengeneza nafasi kwa mchezaji mwingine.

 Ushirikiano wake wa Mwezi mmoja na Kizza miaka miwili iliyopita ulimpatia chati ya juu. Aliibuka mfungaji bora wa Kagame Cup, 2012 akifunga mabao saba katika michezo sita. Baada ya hapo mchezaji huyo amekosa makali. Alionyesha kutojiamini mara baada ya kucheza mfululizo na kushindwa kufunga mabao katika ligi kuu. Amekuwa na misimu miwili mibaya ila kipaji chake kama mshambulizi-mfungaji namba moja wa Kitanzania kinaweza kufufuka. Anakwenda vizuri chini ya Maximo ila ni lazima awe tayari kupambana na Tegete, Hussein Javu na Emmanuel Okwi ambao wamepania kubadilika kimpira na kinadhamu ili kwenda sambamba na mbinu za kocha mpya.

 Katika nafasi hii ni ‘ pasua kichwa’ kwa wachezaji wenyewe na Mwalimu, Maximo ambaye ameamua kumsaini mcheza kutoka Brazil ili kumaliza tatizo la umakini katika ufungaji mabao. Maximo ana wachapa kazi wa kutosha katika timu yake. Okwi amefunga mabao sita katika mechi 13 alizoichezea Yanga, ameanza soka la ushindani mwaka, 2009 na alifunga mabao 17 katika msimu wake wa kwanza katika ligi kuu ya Uganda wakati huo akiwa na miaka 17. Amecheza soka la ushindani kwa miaka mitano tu, kama atacheza mpira na kuachana na mambo mengine ataipendezesha Yanga katika mfumo wa 4-3-3, ila nani akae nje?.

  Kagame Cup itaanza kuonyesha nani na nani watu sahihi wa kuanza katika safu ya mashambulizi. Yanga imekuwa na tatizo la kila mara. Wachezaji kuanza kuchoka dakika 15 za mwisho. Kama watajiandaa zaidi kimazoezi tatizo hilo linaweza kumalizika. Kuziba pengo la Athumani Iddi na Frank Domayo ambalo kwa sasa huwezi kuona uwepo wake ila timu inaposhindwa uwanjani wachezaji hao wanaweza kukumbukwa. Yanga SC, timu ya wananchi yenye uwezo wa kutwaa ubingwa wa sita wa Klabu bingwa Afrika Mashariki na Kati baadae mwezi ujao.

 

 

Post a Comment

AddThis

 
Top