0



Mshambulizi wa Kimataifa wa Tanzania, Mbwana Samatta ameuambia mtandao huu kuwa atatua nchini, tarehe 16 ili kuongeza nguvu katika kikosi cha Taifa Stars.
Samatta ambaye alikuwa na majeraha ambayo yalimfanya aukose mchezo wa marejeano kati ya Tanzania na Zimbamwe, Mwezi uliopita,  kwa sasa yupo fiti japo hajacheza mchezo wowote tangu alipotoka katika maumivu.
 ” Nitakuja kambini tarehe 16 inshallah panapo majaAliwa, naendelea vizuri kwa sasa japokuwa sijacheza mchezo wowote tangu nilipotoka katika maumivu” anasema mshambulizi huyo wakati alipokuwa akiwasiliana na mwandishi wa mtandao huu.

 Samatta, mchezaji wa klabu bingwa mara nne ya Afrika, TP Mazembe ya DRC, amekuwa mmoja wa wachezaji muhimu sana katika timu ya Taifa ya Tanzania katika kipindi cha miaka mitatu sasa na atatua nchini ili kuungana na kikosi hicho cha kocha Martin Nooij katika kambi ya Tukuyu, Mbeya.


Hiyo itakuwa ni muendelezo wa kujiandaa na mchezo wa kuwania kufuzu kwa hatua ya makundi kuwania tiketi ya kucheza michuano Afrika Mwakani nchini Morocco.

Stars itacheza na timu ya Taifa ya Msumbiji, mwishoni mwa wiki ijayo katika mchezo wa kwanza wa hatua ya mtoano na kitendo cha nyota huyo kuwasili nchini kitamaliza hofu ya Watanzania ambao wamekuwa na wasiwasi na upatikanaji wa mchezaji huyo katika timu ya Taifa kutokana na mara kwa mara kuzuiwa na klabu yake.

 Wakati huohuo mshambulizio huyo amesema kuwa timu ya Taifa ya Brazil imepata aibu kubwa baada ya kukubali kipigo cha mabao 7-1 kutoka kwa Ujerumani katika mchezo wa nusu fainali ya kombe la dunia usiku wa kuamikia leo. Brazil ilifungwa mabao hayo ikiwa mwenyeji na kitendo hicho kimemfanya, Samata kusema: ” Hakika Brazil wamepata aibu kubwa sana, ila ndio mpira ulivyo’ alisema kwa ufupi mshambulizi huyo.

 

Post a Comment

AddThis

 
Top