0
Mashabiki wa raisi wa fm academia Nyoshi el sadat jana wamempa makavu live kwenye facebook kwa madai kuwa HAWAMUELEWI

Kauli hizo wamezitoa kwa nyakati tofauti wakati wakikoment post ambazo Nyoshi ali post kwa nia njema tu kwenye face book ili kushea furaha na fansi wake

Lakini hali ikawa tofauti ni baadhi ya baadhi ya mashabiki zake wakawa wakilalamika kuwa raisi huyo ana tabia ya kutojibu maswali ambayo wanamuuliza

lakini yeye mwenyewe alipiga kimya kama mbaya akawawekea uso mbuzi as if  haoni au kana kwamba haelewi kiswahili kama unavoona kwenye picha ya chini alivotulia
                                                         El sadat  Nyoshi

Mashabiki hao wakaenda mbali zaidi eti kama raisi huyo hawezi kujibu msg zao basi aweke mtu wa kuwa anamjibia au asiwe anaweka post atulie tu mmmhhhhhhhh

Wengine walikejeli kwa kile walichokiona na wengine walimpongeza kwa kile kilichoonekana kwenye picha iliyo postiwa na prezdaa huyo na waliyosalia ndio hao ambao walikuwa wakionyesha dhahiri kuwa tabia yake ya ku post vitu on facebook na anapoulizwa maswali hataki kujibu IMEWABOA

Alichopost jana Mr.Prezdaa ni nyumba ambayo bado haijaisha kujengwa sambamba na picha zake zingine moja wapo ni hiyo hapo juu

Na katika picha hizo hakukuwekwa Caption yoyote ila kilichotokea ni pale oohh umechelewa kujenga ulikuwa wapi ooohhh hongera kaka ooohhh tupe ratiba ya band ...hayo ni baadhi ya maswali ya mashabiki hao kwa raisi huyo au unaweza ukamuita baba mapachaambaye hakujibu alipiga kimya

Niliingilia kati na kuwaahidi mashabiki hao kuwa nitamtuma mwandishi wangu aliyeko jijini dar es salaam na kumpa namba ya nyoshi ili amuulize anacholalamikiwa na mashabiki wake lakini kwa bahati mbaya sana mpaka tunaingia mitamboni raisi huyo hakuweza kupatikana kwenye cm yake kiganjani ambayo tunahisi itakuwa ni touch screen....mmmhhhh
SOMA BAADHI YA COMENT ZA MASHABIKI WAKE

Post a Comment

AddThis

 
Top