0

Rais wa Simba sc, Evans Elieza Aveva amekabidhiwa rasmi kijiti cha uongozi klabuni hapo

RAIS wa Simba sc, Evans Elieza Aveva amekabidhiwa rasmi kijiti cha uongozi na mwenyekiti aliyemaliza muda wake, Ismail Aden Rage.
Makabidhiano hayo yalifanyika jana makao makuu ya klabu hiyo, mtaa wa Msimbazi, Kariokoo,  jijini Dar es salaam ambapo viongozi wa zamani na wapya walikutana pamoja kwa ajili ya zoezi hilo muhimu.
Aveva na wenzake walikabidhiwa makaburasha yote na Rage ikiwa ni kuashiria kuingia ofsini rasmi kuanza safari ndefu ya miaka minne ya uongozi.
Nilisikiliza kwa umakini hutuba za viongozi wote wawili,kwa maana ya aliyemaliza muda wake, Rage na rais mpya Aveva.
Katika hotuba ya Rage, niligundua busara kubwa ndani yake. Kubwa ambalo nimeona lina maana kubwa ingawa yote yalikuwa na maana ni kudumisha umoja katika klabu hiyo.
Kumbukumbu za Rage zilikuwa sahihi sana ambapo alieleza kuwa wagombea wote wakati wanapiga kampeni zao kuelekea uchaguzi mkuu uliofanyika juni 29 mwaka huu walisisitiza kudumisha umoja katika klabu hiyo.

Mwenyekiti wa Simba aliyemaliza muda wake, Ismail Aden Rage amemuomba Aveva kutoa msamaha
Aveva alikuwa miongoni mwa wagombea waliosisitiza kudumisha umoja na mshikamano katika klabu ya Simba sc.
Kama wagombea wote walikuwa wanazungumza jambo hili, haihitaji muda na akili nyingi kujua kuwa Simba haikuwa na umoja kwa muda mrefu.
Katika safari ya Rage, kuliibuka migogoro mingi ya kiuongozi, hata wanachama walikuwa na matatizo na uongozi huo.
Mara kadhaa wanachama walithubutu kujaribu kumpindua Rage, lakini majaribio yao yalishindikana kwa mujibu wa katiba. Hata viongozi wengine walifanya majaribio ya kumpindua Rage ikiwemo Joseph Itang`are `Mzee Kinessi`, lakini ilishindikana kwasababu mheshimiwa mbunge alilindwa na katiba ya Simba.
Kutokana na hali hiyo ya kukosekana umoja, kila mgombea aliingia kwa sera ya kurudisha umoja na mshikamano kama ilivyokuwa miaka ya nyuma.
Rage kwa upande wake anatambua kabisa kuwa umoja haukuwepo na ndio maana jana karudia maneno ya wagombea hao kama ishara ya kuwakumbusha.
Alimuomba Aveva kumaliza tofauti zote na makundi yote ikiwa ni pamoja na kuwasamehe wanachama 69 waliosimamishwa uanachama wao baada ya kupeleka masuala ya klabu mahakama ya kawaida.
Rage alimwambia Aveva kuwa anaomba kufikia mkutano mkuu utakaofanyika Agosti 3 mwaka huu awe amefikia maamuzi, hususani kutangaza msamaha kwa wanachama hao.
Kundi la watu 69 ni kubwa sana, na kuna uwezekano wapo wengine nyuma yao ambao hawakufika mahakamani. Kama Aveva ataamua kupambana na kundi hili, basi suala la umoja litakuwa ndoto.
Kwa mujibu wa katiba ya Simba, TFF, CAF na FIFA, ni marufuku masuala ya mpira kupelekwa katika mahakama za kawaida za haki. Ukifanya hivyo unajifungia mwenyewe katika masuala ya mpira.
FIFA wanataka masuala yote ya mpira yatatuliwe kwenye mfumo wake wa sheria na si vinginevyo.
Rage alikiri kuwa Aveva yupo sahihi kuwasimamisha wanachama hao na hajavunja katiba ya Simba.
Ni kweli, hatua alizochukua Aveva ni sahihi wala hakuna tatizo. Lakini kuna busara inatakiwa kutumika kwasababu mambo ya uchaguzi siku zote yanakuwa na mambo mengi.
Kutofautiana ni kawaida. Walienda mahakamani, yawezekana walikuwa na hoja na ndio maana mahakama ilikubali kufungua shauri lao, lakini bado si suala la kulifumbia macho.
Wenzetu Nigeria wameshafungiwa na FIFA baada ya serikali kuingilia masuala ya mpira. Hatupendi kuona klabu wala TFF inafikia huko.
Umoja ni nguzo ya kuifanya Simba iwe imara. Aveva anatakiwa kuifanya Simba iwe moja. Ameingia rasmi madarakani hapo jana, ni jambo la msingi kuanza kila kitu upya.
Migongano yote iliyotokea kwenye uchaguzi inatakiwa kumalizwa kwa busara. Kama itaendelezwe, basi tutegemee kuona makundi tena.

Michael Richard Wambura alienguliwa mara mbili katika uchaguzi wa Simba na suala lake kuleta mpasuko klabuni hapo
Rage alisisitiza kuwa Aveva anatakiwa kuwasamehe wanachama wote waliofanya makosa. Kwa maana hiyo hata Michael Richard Wambura anastahili msamaha huo.
Wambura baada ya kusikia tamko la Aveva kuwasimamisha wanachama 69 likiwemo na suala lake na kusema mkutano mkuu ujao utajadili, alimuomba Aveva kusitisha suala hilo na kutoliendeleza kwasababu litaivuruga Simba.
Kwa bahati mbaya aliongea Wambura, lakini mambo aliyoongea Rage jana yanafanana sana na aliyosema katibu mkuu huyo wa zamani wa FAT.
Baada ya maneno yote hayo, Aveva alimshukuru Rage kwa ushauri huo na akaahidi kulifanyia kazi.
Akaenda mbali kwa kumpongeza Rage kwa kazi kubwa aliyofanya akiwa kiongozi. Akakiri kuwa si jambo jepesi kuongoza klabu kubwa kama Simba.
Mazuri yote ya Rage atayaendeleza ikiwemo suala la Uwanja huko Bunju. Yalikuwa maneno mazuri sana kutoka kwa `Mr. Presidaa` wa Simba.
Kulifanyia kazi alikosema Aveva, binafsi naamini itakuwa ni kuwasamehe. Hiyo ndio busara ninayotegemea kutoka kwa rais huyo wa kwanza katika historia ya Simba.
Si jambo la kupuuza hata kidogo. Ushauri wa Rage ulikuwa mzuri mno. Kuwatenga watu 69 ni jambo baya, yawezekana wakawa zaidi ya hao.
Busara ni kuwasamehe na kuwarudisha kundini kwa amani ili simba ianze kujengwa upya.
Kuendeleza haya, basi sinema zitaendelea kuonekana ndani ya klabu hiyo na matokeo yaliyopatikana kwa miaka mitatu mfululizo hayatakwepeka.
Aveva kazi kwako, Simba ni yako na wewe ndiye kiongozi wa juu zaidi. Jaribu kulitafakari kwa kina ili maamuzi utakayotoa yawe chanya kwa Simba.
Rage hakuwa mbaya kwa kila kitu. Yeye ni binadamu, kukosea ni kawaida kama ilivyo kwa mtu yeyote, lakini ana mazuri mengi, hayo inabidi Aveva apambane nayo kuyaendeleza.
Ni uungwana kuheshimu kazi aliyofanya mwenzako, madhaifu huwa hatusemi kwasababu ndio mambo unatakiwa kuyarekebisha.
Umoja haukuwepo wakati wa Rage, huo ulikuwa udhaifu, sasa Aveva ndiye mtu wa kufuta hilo na kuweza kufanya kazi hiyo, hawa watu 69 wanatakiwa kufikiriwa kwa mtazamo chanya.
- See more at: http://shaffihdauda.com/?p=3377#sthash.ZFwa5tHf.dpuf

Kila la kheria wekundu wa Msimbazi Simba katika kuijenga klabu yenu.

Post a Comment

AddThis

Top