0



unakiwa kumaliza mechi Dar es Salaam
……Mimi ni mshambulizi wa kati
Na Baraka Mbolembole
imu ya Soka ya Taifa ya Tanzania, Taifa Stars itacheza na ile ya Msumbiji, Black Mambas mwishoni mwa wiki ijayo katika uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Stars chini ya Mwalimu,Martin Nooij tayari imeingia kambini,Tukuyu Mbeya, mwanzoni mwa wiki hii ikitokea nchini Botswana ilipokuwa na kambi ya mafunzo ya wiki mbili.
Mchezo huo wa kwanza wa mtoano kuwania nafasi ya kufuzu katika hatua ya makundi kuwania tiketi ya kucheza michuano ya Mataifa Afrika, AFCO 2015, Morocco unataraji kuwa mgumu kwa kila upande.
Msumbiji iliifunga Stars katika mchezo wa mwisho wa hatua ya makundi kuwania nafasi ya kufuzu kwa fainali za Afrika mwaka 2008 nchini Ghana.
 Stars ililazwa bao 1-0 katika mchezo wa kwanza wa mashindano katika uwanja wa Taifa, septemba, 2007, bao maridadi la mpira wa kichwa lililofungwa na aliyekuwa nahodha wa Msumbiji, Tico Tico.
Miaka miwili iliyopita timu hizo zilikutana katika michezo ya mtoano kuwania kufuzu kwa fainali zilizofanyika nchini Afrika Kusini,2013 na Stars iliondolewa kwa changamoto ya mikwaju ya penalti.
“ Mechi ya wiki ijayo itakuwa ngumu, naamini Msumbiji nao watakuja wakiwa wamejipanga kuhakikisha hatupati ushindi katika uwanja wa nyumbani” anasema mshambulizi, Mbwana Samatta ambaye alipoteza mkwaju wa mwisho wa penalti na kuitupa nje Stars. Msumbiji walilazimisha sare ya bao 1-1 katika uwanja wa Taifa,wiki mbili baadaye, Stars iliyokuwa chini ya Kim Poulsen ilipata matokeo kama hayo kabla ya kuchapwa katika mipigo ya penalti.
Samatta, mfungaji bora wa kombe la Shirikisho barani Afrika,2013 akiwa na klabu yake ya TPMazembe ya DRC, amekuwa na uzoefu wa kutosha sasa kuhusiana na michezo ya kimataifa ya mtoano bila shaka mshambulizi huyu anaweza kuisaidia zaidi Tanzania katika mchezo ujao kutokana na mafanikio ambayo tayari yameonekana wakati akiwa katika uwakilishi wa klabu yake.
“ Muhimu siyo kutazama mchezaji mmoja mmoja au timu inacheza kwa kiwango gani, ndiyo wakati mwingine mashabiki wanakuwa wakifurahia mpira tunaocheza, lakini kitu muhimu zaidi ni kufunga mabao ya kutosha” anasema, Samatta wakati alipofanya mahojiano na mtandao huu.
Kila mtu anafahamu kuwa mchezo huo utakuwa mgumu, lakini umefikia wakati ambao Stars inatakiwa kufuzu kwa michuano CAN, katika miaka minne iliyopita timu imeshindwa kufikia lengo hilo katika michuano mitatu tofauti, kuna kitu chochote kimepatikana kutoka kwa wachezaji? Wachezaji wamejifunza nini kutoka katika michuano iliyopita?
“  Kuna kitu kimeongezeka kwa timu na kwa mchezaji mmoja mmoja, hivi sasa wachezaji wa Taifa Stars wanajiamini sana wanapokuwa mchezoni, pasi ni nzuri na unakutana hata katika eneo letu la ulinzi wachezaji wanakuwa na utulivu,  wanapasiana bila hofu yoyote. Tunacheza vizuri nyumbani na huwa tunafanya hivyo katika michezo ya ugenini” anasema mshambulizi huyu namba moja wa TP Mazembe. Na kuongeza ;” Kinachotakiwa ni ‘Kutwist’  vichwa vya wachezaji ili waelewe majukumu yao na kuifahamu vizuri timu pinzani, hili ni jukumu ambalo linatakiwa kufanywa na waandishi wa habari pia. Inasaidia kuwafanya wachezaji waelewe mchezo ulio mbele yao”
Tanzania ilitolewa na Msumbiji miaka miwili iliyopita katika michuano kama hii, ili kufuzu kwa fainali za Morocco,Stars inalazimika kuitoa kwanza ,Black Mambas ili kuungana na timu za Zambia, Niger na Cape Verde kuwania tiketi mbili za kundi hilo ambazo zinaweza kupatikana, lakini kwa kulipa kisasi cha timu hiyo ya Kusini mwa Afrika.
 

 
Kwanza ni lazima tumalize mechi Dar es Salaam,hatutakiwi kufanya kama wakati ule tuliposhindwa kupata ushindi katika uwanja wa nyumbani” anasema Samatta ambaye amekuwa akipangwa katika nafasi ya mshambulizi wa pembeni au mshambulizi wa pili katika timu ya Taifa. Samatta amefunga mabao sita katika michezo17 inayotambulika na FIFA kuanzia mwaka 2011 alipoitwa kwa mara ya kwanza na kocha Jan Poulsen.
Poulsen alimuingiza kikosini akiwa na miaka 18 na haraka akamuamini kama mshambulizi wa kwanza katika kikosi chake. Alifunga mabao manne ndani ya mwaka mmoja aliofanya kazi na Jan lakini tangu timu hiyo ikinolewa na Kim Poulsen, Samatta amekuwa ‘butu’ katika ufungaji japokuwa amekuwa mfungaji wa kutegemewa sana katika klabu yake ya TP Mazembe.
“  Nachoweza kusema nimekuwa makini na mtulivu, na wakati mwingine huwa nasema ni bahati kutoka kwa Mungu. Mimi ni ‘ mwanajeshi wa mbele’ mshambulizi wa kwanza kabisa, hivyo ndivyo ninavyotumika katika klabu yangu na nimekuwa nifunga mabao ya kutosha kutokana na kupangwa katika nafasi hiyo nayoipenda. Mchezaji huwezi kujichagulia nafasi ya kucheza katika timu, mahitaji ya Mwalimu ndiyo jambo la msingi. Napenda kucheza katika nafasi yoyote nayopangwa Stars kutokana na mfumo wa kocha anavyotaka” anasema Samatta amekuwa akipangwa nyuma ya mshambulizi, John Bocco katika timu ya Taifa


“ Siwezi kusema kama huwa nina furaha au laa!, naweza kufurahia kama nikipangwa katika wingi ya kushoto, au mshambulizi wa kwanza na si nyuma ya mshambuliaji wa kwanza kwa sababu nakosa nafasi ya kuuchezea mpira”
Naweza kufurahi km nikicheza km winga ya kushoto au streka sio nyuma ya streka
Mechi 17 za Fifa, mabao sita inamaanisha nini kwa mshambulizi huyu unayependwa nchini Tanzania. “ Bado sijafanya nachopenda kufanya, lakini inatokana na ufinyu wa michezo, bado nina imani wakati upo wa kufanya mambo makubwa kwa Taifa langu, kufunga mabao kadri inavyowezekana ili kukaribiana idadi ya michezo”anasema mchezaji huyo anayedai anafunga mabao mengi katika klabu yake kutokana na kuzungukwa na wachezaji wengi wa kulipwa, kitu ambacho hakipo kwa Stars.
Samatta ametoa wito kwa mashabiki wa soka nchini kuwapa sapoti wachezaji wao katika muda wote wa mchezo na kuwafanya wageni wao kuingia mchecheto. Hivyo ndivyo mazingira ya uwanja yanavyokuwa katika uwanja Stade de TP Mazembe wakati timu ngeni zinapokuwa zikitembelea katika uwanja huo.
“ Mashabiki wana mchango mkubwa sana katika mchezo kama huo,wanatakiwa kuinuka katika viti vyao na kuimba wimbo wa Taifa pamoja na wachezaji. Kuishangilia timu muda wote ili kuwafanya Msumbiji wajione wapo ugenini hasa. Waje kwa wingi uwanjani siku ya mchezo kuipa sapoti timu”



Post a Comment

AddThis

 
Top