0

KOCHA mkuu wa Yanga sc, Mbrazil, Marcio Maximo kesho anaweza kuwataja wachezaji atakaowatumia katika michuano ya kombe la Kagame itakayofanyika mjini Kigali, Rwanda kuanzia Agosti 8 mwaka huu.
Katibu mkuu wa Yanga, Beno Njovu amesema Maximo atazungumza na waandishi wa habari kesho baada ya mazoezi katika uwanja wa shule ya sekondari ya Loyola, Mabibo jijini Dar es salaam, hivyo anaweza kudokeza wachezaji atakoenda nao Rwanda.
“Kesho mwalimu ataongea  na waandishi wa habari, kwahiyo yawezekana akatoa dalili ya wachezaji gani anaweza kuwatumia  kombe la Kagame,” alisema Njovu.
“Hasa ukizingatia mwishoni mwa wiki timu nyingi za taifa zitakuwa na mechi, kwahiyo yawezekana wachezaji wengi wakawa hawajawasili, mpaka terehe ya safari yetu, hivyo mwalimu akashindwa kuwatumia.
Njovu alisema kwa vile michuano inaanza Agosti 8, wanajipanga kuondoka nchini Agosti 5, ingawa bado hawana uhakika.
Kuhusu mchezaji wa kigeni atayeachwa kati ya Emmanuel Okwi, Khamis Kiiza na Haruna Niyonzima baada ya kusajiliwa kwa Wabrazil wawili, Andrey Coutinho na Gleison Santos Santana ‘Jaja’,  Njovu alisema mpaka sasa mwalimu hajafikia mamuzi ya nani anapunguzwa.
“Mwalimu atathibitisha baada ya kuwaona wachezaji hawa wote wakifanya mazoezi pamoja na kuona ni kombinesheni ipi itamfaa, hapo ndipo ataamua ni mchezaji gani anaachwa, hata kama itasikitisha”
“Bado muda tunao, mwalimu anaweza kumtema mchezaji hata baada ya kombe la Kagame kwa maana ya kwamba atakuwa amepata muda mzuri wa kuwaona wachezaji hao”. Aliongeza Njovu.

Post a Comment

AddThis

 
Top