Katika kesi hiyo inayoendeshwa na Hakimu Wilbert Luago,amelazimika kuhairisha kesi hiyo kwa muda wa nusu saa kwa hoja aliyoitoa Mbasha kwamba ana wakili wa kumtetea lakini alishindwa kufika kutokana na matatizo ya usafiri.
Kauli hiyo ya Mbasha ilimfanya Hakimu Luago kuhoji kama kweli alikuwa na nia ya kuwa na wakili au ana nia ya kuweka wakili kwani ilionekana tangu kesi hiyo ianze Mbasha hakuwai kusimamiwa na wakili.
Mara baada ya nusu saa kupita Wakili wa mshitakiwa alituma muakilishi wake kuwakilisha barua za dharula ambazo zilionesha kuwa yupo safarini mkoani Arusha na kuomba kesi hiyo kuahirishwa.
Emanuel Mbasha ana kabiliwa na kesi mbili za ubakaji ambapo inadaiwa alitenda makosa hayo maeneo ya Tabata katika nyakati mbili tofauti,Mbasha alisindikizwa mahakamani na ndugu zake huku Mkewe Flora Mbasha kutoonekana Mahakamani na badala yake alionekana mdogo wake Flora ambaye ni shemeji yake Emanuel Mbasha.
Kesi hii imehairishwa mpaka July 23 mwaka huu .
Post a Comment