Mchungaji Semeni alinaswa akiwa na mwanamke huyo aitwaye Erizabert Kisanda, mkazi wa jijini Mwanza ambaye alifika Dar kuonana naye kwa ajili ya kumwombea maombi maalum ya kiroho ‘deliverance’ kutokana na matatizo ya mke huyo kushika mimba na kutoka kila wakati.
“Huyu mwanamke alikuja Dar kwa mchungaji kwa lengo la kuombewa apate mtoto. Alikuwa na tatizo la uzazi kwani kila alipopata ujauzito, akikaribia kujifungua tu mimba inaharibika.
“Kutokana na tatizo hilo, ndipo akashauriwa akamwone mchungaji huyo ndipo akafunga safari kwenda kumuona na kumweleza tatizo lake, mchungaji akamwambia ni tatizo dogo sana kwake.” Anasimulia shuhuda wa mkasa huo.
Ilizidi kudaiwa kwamba, ahadi ilipangwa ambapo mwanamke huyo alitakiwa kurudi siku hiyo ya tukio.
Ilizidi kudaiwa kwamba, ahadi ilipangwa ambapo mwanamke huyo alitakiwa kurudi siku hiyo ya tukio.
Siku ya tukio, mwanamke huyo alifika kuombewa ambapo mchungaji huyo alizama kiroho zaidi kwa muda wa saa mbili.
“Baada ya kumaliza maombi hayo ndani ya kanisa ndipo mchungaji huyo akamchombeza kwa kumwambia wazame chumbani akamwombee zaidi,” chanzo kilisema.
“Baada ya kumaliza maombi hayo ndani ya kanisa ndipo mchungaji huyo akamchombeza kwa kumwambia wazame chumbani akamwombee zaidi,” chanzo kilisema.
Habari zaidi zinadai kuwa wakiwa chumbani sasa, mke hana nguo, mchungaji akiwa ndani ya kipensi tu, mwanaume aliyedaiwa ni mume na dada yake walitokea kusikojulikana na kuwavaa, hali iliyosababisha tafrani kubwa.
Kuhusu kilichotokea baadaye baada ya fumanizi hilo ni kwamba kanisa hilo limefungwa. Mara baada ya waumini wake kuona fumanizi la baba mchungaji huyo walisusa kwenda kanisani hapo.
Habari zilizonaswa kutoka kanisani hapo kutoka kwa muunini mmoja zilidai kuwa baba mchungaji huyo ameingia mitini na hajulikani alipo.
“Ilikuwa ni aibu kubwa sana kwa mtumishi wa Mungu. Baada fumanizi lile, baba mchungaji hajaonekana tena na kanisa limefungwa,” alisema mmoja wa waumini hao
Post a Comment