0

Kama timu ina uwezo wa kupanga mashambulizi na haitengenezi nafasi za kufunga kutokea katikati ya uwanja hilo ni tatizo, pasi za mabao msingi wake unatoka katika eneo la kiungo. Katika mchezo wa kwanza wa hatua ya mtoano kuwania nafasi ya kufuzu kwa hatua ya makundi ya kuwania nafasi ya kufuzu kwa fainali za kombe la Mataifa ya Afrika, AFCON, 2015, Morocco kati ya Tanzania, Taifa Stars na Msumbiji, Black Mambas ambao ulifanyika katika uwanja wa Taifa, Dar es Salaam, siku ya Jumapili na kumalizika kwa sare ya kufungana mabao 2-2.

 Kocha wa Stars, Martin Nooij aliwaanzisha washambuliaji wanne, huku watatu kati yao wakiwa na uwezo mkubwa wa kucheza katika safu ya mshambulizi wa kati. Mrisho Ngassa alipangwa katika nafasi ya winga wa kushoto, nafasi ambayo kiuhalisia ilifungua milango yake ya mafanikio katika soka la Tanzania. Thomas Ulimwengu alipangwa katika winga ya kushoto, nafasi ambayo kutokana na uhaba wa wachezaji imekuwa wazi, Tom, ameendelea kucheza kwa kiwango kizuri katika timu ya Taifa. John Bocco alipangwa kama mshambulizi wa kwanza na mshambuliaji huyo aliendelea kuwa na kiwango cha chini katika timu ya Taifa. Mbwana Samatta alipangwa katika nafasi ya mshambuliaji namba mbili akicheza nyuma ya Bocco. Samatta alijaribu kucheza kama mchezesha timu, akishuka hadi katikati ya uwanja na kutawanya pasi za kwenda mbele.
  Kiujumla wachezaji wote wanne walicheza vizuri, lakini majukumu waliyotakiwa kuyafanya ili timu kupata mabao hawakuweza kuyatimiza. Sababu ni nyingi ambazo zilifanya wachezaji hao kutooneka uwanjani kwa muda mrefu wa kipindi cha kwanza. Kwanza, ni namna timu ilivyokuwa inacheza kwa mwendo wa taratibu ambao hauwafanyi wapinzani kucheza kwa kufungua nafasi. Stars haikucheza kwa kasi.
 Mambas walikuwa na mchezaji mmoja tu wa hatari katika kikosi chao, nahodha na kiungo mchezesha timu, Elias Pelembe ‘ Dominguez’, lakini Stars ilikuwa na faida kwa sababu mchezaji huyo tayari amekuwepo katika mipambano minne kati ya kumi ya mwisho baina ya timu hizo. Mambas walionekana kucheza kwa tahadhari kubwa kuanzia safu ya ulinzi hadi ile ya mashambulizi. Mabeki wao walijitahidi kuwakaba, Bocco na Samatta, na walikuwa makini kuhakikisha, Ngassa na Ulimwengu hawatumia mbio zao kuingia na kufunga mabao wakitokea pembeni. ‘ Pasi mkaa’ zilikuwa nyingi, ilifikia wakati mlinzi wa kulia wa Stars, Shomari Kapombe akirusha mpira kwa mchezaji wa Msumbiji.
 Ni dalili ya kutokujiamini hata katika uwanja wa nyumbani. Mambas, walikuja Tanzania huku wakiamini wanakuja kucheza na timu bora. Japokuwa walikuwa na wachezaji wanaocheza soka la kulipwa barani Ulaya na nchini, Afrika Kusini walionyesha wasiwasi nusu saa ya kwanza ya mchezo. Stars ilikuwa na wachezaji bora vijana jambo ambalo lilimpatia hofu kocha wa Mambas… Ila, ajabu wachezaji wa Stars walikosa kujiamini katika kumiliki mpira na kupiga pasi. Kitu kizuri ni kwamba jambo hilo lilianza kutoweka kadri muda ulivyokuwa ukisonga mbele.
 Mlinzi wa kati na nahodha wa Stars, Nadir Haroub  ‘ nusura’ afunge mara mbili katika kipindi cha kwanza. Uchezaji wa Nadir katika kipindi cha Miezi Sita sasa kimekuwa ni cha juu mno. Namna alivyopanda na ‘ move’ ya mpira hadi kuwa mpigaji wa mwisho wa krosi umenikumbusha kiwango cha mlinzi wa zamani wa Kimataifa wa Ufaransa na klabu za Chelsea, Arsenal na Tottenham, William Gallas. Nadir ni ‘ kiongozi wa ukweli’. Kama wachezaji wote wangewajibiki kwa kiwango kama cha Nadir, mechi ilikuwa nafuu kwa upande wa Stars, na pengine mabao mawili waliyopambana kuyapata katika dakika 43 za kipindi cha pili wangeyapata katika kipindi cha kwanza na kumalizia mechi katika nusu ya pili ya mchezo.
- See more at: http://shaffihdauda.com/?p=3805#sthash.THu5FPiB.dpuf

 Aliendelea kusema kwa kujiamini kuwa yeye ni ‘ mwanajeshi wa mbele’ akimaanisha anafunga mara kwa mara akiwa klabuni, TP kwa sababu anapangwa katika nafasi ya mshambuliaji wa kwanza. Umeona anavyotumika, Stars?. Kim Poulsen alikuwa ana muharibu kwa kumpanga mbali na goli, ukitazama mabao yake sita aliyofunga katika michezo 20 akiwa na Stars, manne aliyafunga wakati wa Jan Poulsen ambaye alimuamini haraka akiwa na miaka 19 na kumtambulisha kama mfungaji namba moja wa Tanzania, Machi, 2011 alipomuinua katika benchi na kwenda kuifungia, Stars bao la ushindi wakati huo katika mchezo wa kuwania nafasi ya kufuzu kwa fainali za Afrika 2012, Equator Guinnea na Benin.

Si kwamba hafurahi kupangwa katika nafasi tofauti katika timu ya Taifa, Samatta aliniambia wazi kuwa hapendi kucheza kama mshambuliaji wa pili, anapenda kuuchezea mpira na kufunga mabao hivyo nafasi pekee inamfanya kuwa huru uwanjani ni mshambulizi wa kwanza. Aliniambia wazi kuwa hapendezwi na takwimu zake mbaya katika soka la kimataifa, ila kama mchezaji anajitahidi kuendana na falsafa za Mwalimu na kucheza kadri anavyotakiwa. Timu imara katika kujilinda ni ile yenye uwezo wa kufunga mabao na kumiliki mpira kwa muda mwingi.

 Endapo, Bocco atatumia uzoefu wake wa miaka mitano kama mchezaji wa timu ya Taifa anafaa kuwa mshambulizi namba moja, kutokana na umbo lake, shabaha yake ya kufunga mabao, Bocco ni mchezaji wa hatari, ila kwa kiwango chake alichoendelea kukionyesha katika mchezo uliopita ni wakati sahihi wa Samatta kupangwa katika nafasi hiyo. Dominguez ni winga kama ilivyo kwa Ngassa ila kutokana na thamani ya mchezaji huyo amekuwa akitumika kama silaha ya kwanza kujilinda, ni mchezaji ambaye maarifa yake binafsi tuliyaona miaka saba iliyopita wakati alipompiga chenga maridadi, Amir Maftah na kupiga krosi sahihi kwa Tico Tico.
 Huyu ni mchezaji anayelipwa pesa nyingi katika ligi kuu ya Afrika Kusini akiichezea klabu tajiri ya Mamelodi Sundowns , PSL, ni mchezaji bora wa mwaka wa PSL na mshindi wa taji hilo akiwa na Super Sports United. Silaha ya Stars inafichwa na mbinu za Nooij wakati Samatta ni mshambuliaji wa saba kwa ubora barani Afrika.

Samatta arudishwe katika nafasi ya mshambuliaji wa kwanza, Ulimwengu anaweza kuendelea kutumika kama mshambuliaji wa pembeni na nyuma ya Samatta apangwe ‘ mchezaji wa maajabu’ Hamis Mcha ‘ Vialli’, Ngassa ameshuka kiwango, winga ya kulia ni nafasi ya Saimon Msuva, timu ikimbie uwanjani na wachezaji wapunguze kupiga pasi zisizofika. Kufunga mabao mawili ugenini inawezekana kwa sababu, Mambas wanawahofia, Samatta na Tom, ila wasiwasi wangu kama kweli hatutaruhusu mabao. TFF waende Msumbiji kujifunza namna ya kuwavutia mashabiki uwanjani,sikwa kuuza tiketikatika simu za mkomm bali kwa kuweka viingilio vya chini ili mashabiki wajitokeze kwa wingi. Tulijifunza nini kutoka kwa Zimbabwe?. Mambas wamepata walichotaka ila tunaweza kufikja malengo yetu tukiwa ugenini.
 
Post a Comment

AddThis

Top