0


Usajili wa mchezaji wa nafasi ya golikipa ambao, Simba SC wameufanya katika kipindi cha miezi sita hadi saba hivi sasa umekidhi viwango vya mchezaji anayeweza kufuata nyayo za walinda mlango mahiri ambao walikuwa msingi wa mafanikio ya timu hiyo katika miaka ya nyuma.

 Ivo Mapunda alisajiliwa Mwezi, Disemba akitokea klabu ya Gor Mahia ya Kenya, kwa muda wa nusu msimu aliofanya kazi Simba, Ivo amekutana na changamoto za hapa na pale.

 Matatizo ya kifamilia ikiwemo kifo cha baba yake mzazi, kiwango cha Ivo kilianza kutia shaka wakati alipofungwa bao la mbali na Mussa Hassan ‘ Mgosi’ katika mchezo wa ligi kuu mzunguko wa pili dhidi ya Mtibwa Sugar katika uwanja wa Jamhuri, Morogoro. 

Baada ya kuanza vizuri katika mchezo wa hisani dhidi ya mahasimu wao, Yanga SC mwishoni mwa Mwaka uliopita, Ivo aliendelea kuwa na kiwango cha kuvutia katika michezo ya Mapinduzi Cup huko, Zanzibar na aliisaidia sana, Simba kufika fainali ya michuano hiyo hiyo.
Akicheza na safu mpya ya ulinzi, Ivo alikuwa ameruhusu mabao matatu tu hadi wanakutana na Mtibwa, Februari 5. Baada ya hapo alifanya makosa katika mchezo dhidi ya JKT Mgambo na kuanza kushutumiwa kuwa anaifungisha Simba kwa sababu amewahi kucheza Yanga. Hayo si mambo mageni katika soka la Tanzania hasa mchezaji anapokuwa katika timu za Simba na Yanga.
 Acha na Yaw Berko, Simba awali haikupaswa kuwa na Abel Dhaira na haipaswi kuwa na golikipa kutoka nchi ya nchi. Baada ya kumaliza katika nafasi ya nne msimu uliopita ni wazi ilihitaji mabadiliko makubwa ya wachezaji. Nafasi ya golikipa ilikuwa ni muhimu na kitendo cha kuwasaini, Hussein Shariff na chipukizi Manyika Peter Manyika ni ishara njema kuwa timu imejidhatiti kuinuka na kurejea katika mwendo wa ushindani wa ubingwa. Shariff ndiye kipa bora wa msimu ulipita, tuzo aliyoipata baada ya kucheza kwa kiwango cha juu katika michezo zaidi ya 20 akiwa na Mtibwa.
- See more at: http://shaffihdauda.com/?p=3852#sthash.8ogOScmx.dpuf

Akicheza na safu mpya ya ulinzi, Ivo alikuwa ameruhusu mabao matatu tu hadi wanakutana na Mtibwa, Februari 5. Baada ya hapo alifanya makosa katika mchezo dhidi ya JKT Mgambo na kuanza kushutumiwa kuwa anaifungisha Simba kwa sababu amewahi kucheza Yanga. 

Hayo si mambo mageni katika soka la Tanzania hasa mchezaji anapokuwa katika timu za Simba na Yanga.

 Acha na Yaw Berko, Simba awali haikupaswa kuwa na Abel Dhaira na haipaswi kuwa na golikipa kutoka nchi ya nchi. Baada ya kumaliza katika nafasi ya nne msimu uliopita ni wazi ilihitaji mabadiliko makubwa ya wachezaji. 
Nafasi ya golikipa ilikuwa ni muhimu na kitendo cha kuwasaini, Hussein Shariff na chipukizi Manyika Peter Manyika ni ishara njema kuwa timu imejidhatiti kuinuka na kurejea katika mwendo wa ushindani wa ubingwa. 

Shariff ndiye kipa bora wa msimu ulipita, tuzo aliyoipata baada ya kucheza kwa kiwango cha juu katika michezo zaidi ya 20 akiwa na Mtibwa.

Shariff amecheza Mtibwa kwa miaka miwili kama mbadala wa Deo Munish. Alikuwa chaguo la kwanza tangu kuondoka kwa Shaaban Kado aliyekwenda, Coastal Union wakati wa usajili wa dirisha dogo msimu wa 2012/13.


 Tayari, Ivo amesema anamkaribisha, Hussein katika vita ya ushindani wa namba huku akimtaka kujifunza mbinu mbalimbali za ugolikipa kutoka kwake. Ivo mchezaji aliyepevuka kiakili na kiumri, ni golikipa wa muda mrefu ambaye amecheza chini ya Walimu wengi wa kimataifa hivyo ni mchezaji ambaye anaweza kuwa ‘ Mwalimu wa Ziada’ kwa Hussein na Manyika ambao pia wamewahi kuziwakilisha timu za Taifa.

 Simba imefanya usajili mzuri katika nafasi ya golika. Idara ambayo imekuwa ni msingi wa mafanikio ya vikosi vilivyopita. Ligi ya msimu ujao itakuwa ni ngumu sana tofauti na ilivyokuwa msimu uliopita. 

Hivyo timu yenye wigo mpana wa wachezaji bora itakuwa na nafasi kubwa ya kufanya vizuri hata kama baadhi ya wachezaji watashikwa na uchovu au majeraha mambo ambayo hayahepukiki katika ligi yenye ushindani.

 Timu bora huanza kujengwa katika safu ya ulinzi na nafasi golikipa ni muhimu zaidi. Sasa ni jukumu la wachezaji wenyewe kuzidisha na kudumisha mahusiano yao ya kizazi huku kika mmoja akichukua mbinubora za mwenzake. Kama kila mmoja atajituma na kufanya vizuri katika mazoezi kuna nafasi ya wachezaji wote hao watatu kucheza. 

Simba imefanya usajili ambao mchezaji ukilala mwenzako anachukua nafasi. Ivo Mapunda vs Hussein Shariff hii ni vita ya kuimarisha idara ya ulinzi na kujenga msingi imara wa timu. Wakilala itakuwa nafasi ya Manyika
 


Post a Comment

AddThis

 
Top