Unapouzuru mji wa Malindi uliopo kwenye mwambao wa Kenya unaonekana kama paradiso.
Hata hivyo mji huu ni kitovu kilichojificha cha biashara ya ngono ya watotoWatoto wadogo wenye umri wa miaka hata 12 hutumiwa katika ukahaba na filamu za ngono na watalii ambao huwa tayari kulipa pesa nyingi kwa ajili ya ngono katika maeneo yaliyojificha .
Maafisa wanasema biashara hii imependwa sana na wasichana hao wadogo na wavulana kiasi kwamba wengi wao huacha shule .
Kijana mmoja mwenye umri wa miaka kumi na saba ameiambia BBC kuwa aliacha shule kutokana na ufukara.
Alivutiwa kuingia katika biashara ya ngono baada ya rafiki yake aliyekuwa akifanya kazi hiyo kukutana na mtalii aliyempeleka bara Uropa na sasa anaishi maisha ya ustaarabu.
Maisha ni hayo hayo pia kwa wasichana.
Msichana mmoja ameiambia BBC kuwa alianza biashara ya ngono akiwa na miaka 15, bila mamake kujua.
Anaeleza ugumu wa biashara hiyo na jinsi wasichana wanavyogeuzwa kuwa watumwa wa ngono na hata kulazimishwa kushiriki tendo hilo na wanyama kama mbwa.
Hatahivyo anasema haoini ubaya wowote kwani ndiyo njia pekee inayomuwezesha kujimudu kimaisha.
Juhudi za mamake kumshawishi aiache biashara hiyo zimeambulia patupu.
Ni suala linalowasumbua viongozi katika jamii hii. Naibu chifu wa kata ndogo ya Shela, Mayele anasema watu wengi hawatoi ripoti kwa serikali.
Sasa Chifu huyo ameanzisha harakati kwa jina ''rudi shule'' ambapo watoto wakipatikana mjini wakati wa shule wanakamatwa na kupelekwa nyumbani, kisha wazazi wao kukamatwa na kufunguliwa mashtaka.
Anaamini kwamba mambo yataimarika, lakini changamoto bado ni nyingi.
Post a Comment