0
Mazungumzo: Ryan Giggs (pichani akiwa na mke wake Stacey mjini Manchester) alikuwa Uholanzi kukutana na Louis van Gaal.


RYAN Giggs leo mchana alikuwa nchini Uholanzi kwa ajili ya kufanya mazungumzo na kocha mtarajiwa wa Manchester United, Louis van Gaal.

Kocha huyo wa muda wa Man United alitakiwa kukutana na Mholanzi huyo mjini Noordwijk, karibu na Hoteli ambayo timu ya Uholanzi inafanya mazoezi, na wawili hao walitakiwa kukutana ili kujadili hatima ya baadaye ya Man United.

Giggs mwenye miaka 40 alionekana akitoka katika hoteli ya Van Oranje mchana wa leo. Mkurugenzi mkuu wa Man United, Ed Woodward alitakiwa pia kuwepo katika kikao hicho
 Giggs alitakiwa kukutana na Van Gaal kujadili hatima yake ya baadaye katika klabu ya Man United
 Sehemu ya mkutano: Hoteli ya Van Orange mjini, Noordwijk ndio sehemu ambayo Giggs alitakiwa kukutana na Van Gaal
Mtarajiwa: Van Gaal anatarajiwa kutangazwa kuwa kocha wa Man United wiki hii.

Post a Comment

AddThis

 
Top