0


i. Phyllis Schalafly (pichani), ambaye ni mwanzilishi wa kitengo maaarufu cha wanaharakati wanaopinga harakati za wanawake dhidi ya wanaume ‘Anti-feminist Eagle Forum’ cha Washington, Marekani ameiomba serikali ya Washington isitishe suala la kujaribu kuwalipa ujira sawa wanawake na wanaume.
Akielezea sababu kubwa ya kutoa ushauri huo, mama huyo amesema kuwa wanaume wengi hawapendi kuwa katika ndoa na wanawake ambao wanapata kipato sawa ama zaidi na kile wanachokipata.
Mwanaharakati huyo ameandika maelezo yake kwa kuegemea pande zote mbili ambapo kwa lugha ya kitaalamu ameitaja hypergamy kuwa moja ya sababu zake.

“Sababu nyingine ni ushawishi wa hypergamy, ambayo inamaanisha kuwa wanawake huchagua wanaume wa ndoa ama wapenzi ambao wanaingiza pesa nyingi zaidi yao.” Ameandika mama huyo kwenye kipeperushi kilichosambazwa na Right Wing Watch.

“Wakati wanawake wanataka kuoelewa na wanaume wenye kipato kikubwa, wanaume kwa ujumla wanapenda kuwa wenye kipato kikubwa zaidi katika uhusiano kuliko wanawake.” Ameongeza.

Amefafanua kuwa hali hiyo ya kutopata ujira sawa inaweza kuwa na madhara lakini ni afadhali kuliko madhara yatakayopatikana kwenye ndoa ama kimahusiano kutokana na kutokuwepo na utofauti wa kipato.

 Mwezi mmoja uliopita, mwanaharakati huyo mwanamke alieleza kuwa kuna umuhimu wa kutofautisha kazi za wanawake na kazi wanazofanya wanaume kwa kuwa kiuhalisia wanaume wanaweza kufanya kazi kwa muda mrefu na hata wiki nzima wakati wanawake wanapenda kufanya kazi hiyo hiyo kwa muda mfupi.

Hata hivyo, amekiri kuwa wapo wanawake wachache ambao wanapenda kufanya kazi kwa muda na aina ile ile kama ifanywavyo na wanaume.

Post a Comment

AddThis

 
Top