0


Baada ya kutapakaa kwa picha ya matukio ya utengenezaji wa video ya wimbo wa 50 Cent, 50 alichukua uamuzi wa kuandika katika akaunti yake ya instagram yenye wafuasi zaidi ya milioni 8 na kumkashifu video queen aliekuwa akifanya nae kazi katika video hiyo kwa kumtuhumu kuwa yeye ndio amesambaza picha hizo.

kupitia Instagram na twitter 50 aliandika aliwaonya watu wasifanye kazi na mwanadada huyo na kumuita malaya mwenye kiu na video,
 "WARNING: Do not attempt to work with this thirsty video bitch."
 
Sally Ferreira pia amemshitaki 50 kwa kumkashifu na kudai kuwa amemshutum visivyo mwezi uliopita kuwa amekuwa akisambaza uvumi kuwa  ana date na 50 

Kwa upande wake Sally anasema hajawahi kusambaza picha hizo na kusisitiza kuwa amekuwa katika mahusiano ya wazi na mchumba wake kwa miaka 9
Ferreira anadai kuwa 50 kupost shutuma hizo, ambazo alizifuta sio tu kazi yake ya modeling, bali amemuingiza katika kejeli zisizoisha kutoka kwa watu. Matokeo yake ameathirika kihisia na anataka milioni kadhaa kama fidia 

Post a Comment

AddThis

 
Top