JOSE Mourinho kesho usiku atavunja rekodi ya aliyekuwa kocha wa Manchester United, Sir Alex Ferguson kufika nusu fainali mara nyingi zaidi katika michuano ya UEFA ambapo atakabiliana na Atletico Madrid.
Nusu fainali ya kesho itakuwa ya 8 kwa Mreno huyo na nusu fainali ya tatu akiwa Stamford Bridge, wakati Ferguson katika maisha yake Old Trafford alifika hatua ya nusu fainali ya ligi ya mabingwa barani Ulaya mara 7.
Mourinho katika historia yake ya kufundisha soka alianza kucheza UEFA msimu wa 2001/2002 baada ya kupewa nafasi ya kocha wa muda wa FC Porto ambapo alienda na timu msimu mzima.
UEFA ya 2004, Mourinho alitinga fainali na kutwaa `ndoo` Old Trafford.
Hiyo ndio ilikuwa nusu fainali ya kwanza kwa kocha huyo na baadaye aliondoka zake kujiunga na Chelsea.
Mwaka 2005 na 2007 aliifikisha Chelsea katika hatua ya nusu fainali ya kombe la Ulaya `Cups of European Glory`, lakini alitolewa na Liverpool katika miaka hiyo hatua ya nusu fainali.
Baada ya hapo, Mourinho aliondoka Chelsea na alikaa bila timu kwa muda mrefu kabla ya kukubaliana kuifundisha Inter Milan.
Katika msimu wake wa kwanza alifanikiwa kubeba kombe la ligi kuu nchini Italia, Seria A, lakini hali ilikuwa mbaya michuano ya UEFA baada ya kutolewa hatua ya 16 na Manchester United ya Alex Ferguson.
Hata hivyo msimu wa 2009/2010, Mourinho alifanikiwa kutwaa mataji matatu ndani ya msimu mmoja akiwa na Inter Milan.
Alibeba taji la ligi kuu, kombe la Coppa Italia na UEFA. Haya yalikuwa mafanikio makubwa kwa Inter Milan tangu mwaka 1965.
Mwaka huo, ilikuwa nusu fainali ya nne ya UEFA kwa Mourinho na ubingwa wa pili wa michuano ya UEFA.
Akiwa na Real Madrid kwa miaka mitatu mfululizo, Mourinho alifanikiwa kutinga hatua ya nusu fainali na kufikisha nusu fainali 7.
Sasa ya kesho inakuwa fainali ya 8 kwake na atakuwa amevunja rekodi ya kibabu Sir Alex Ferguson aliyecheza nusu fainali 7.
Sir Ferguson aliiongoza Man United hatua ya nusu fainali mnamo mwaka 1997, 1999, 2002, 2007, 2008, 2009, na 2011.
Mourinho yeye ametinga fainali kwa mwaka 2004, 2005, 2007, 2010, 2011, 2013, 2013 na mwaka huu 2014.
Makocha wengine wanaofuatia kutinga nusu fainali ya UEFA mara nyingi na klabu walizokuwa nazo kwenye mabano ni wafautao
Marcello Lippi (Juventus) alitinga mara 5 kuanzia mwaka 1996, 1997, 1998, 1999 na 2003.
Migeul Munoz ( Real Madrid)naye alitinga mara 5 kwa mwaka 1960, 1964, 1966, 1968 na 1973.
Louis van Gaal ( Ajax, Barca, Bayern) aliingia nusu fainali mara 5 mnamo mwaka 1995, 1996, 1997, 2000 na 2010.
Pep Guardiola naye amecheza nusu fainali 5 ambazo ni mwaka2009, 2010, 2011, 2012 na mwaka huu 2014.
Post a Comment