0

Siku chache baada ya gazeti ya gazeti moja la michezo kuripoti kwamba golikipa Juma Kaseja na beki Kelvin Yondani wametajwa kuchukua fedha kutoka kwa klabu ya Azam FC ili waifungishe timu yao kwenye mchezo waliopata kichapo dhidi ya Mgambo JKT - meneja wa kipa Juma Kaseja amezungumza na mtandao huu na kutoa ahadi ya kulipeleka gazeti hilo mahakamani.

Akizungumza na mtandao huu meneja wa Kaseja Abdulfatah Saleh alisema kwamba kwamba gazeti hilo limemchafulia jina na sifa mteja wake, na hivyo ameshauriana na Kaseja na sasa wamefikia maamuzi ya kwenda mahakamani kulishtaki gazeti kwa kuripoti story ya uongo dhidi ya kipa huyo ambaye alikaaa kwenye lango la Yanga kwenye mchezo dhidi ya Mgambo na wanajangwani wakafungwa
mabao 2-1 hivyo kuuweka ubingwa wao rehani.

"Taarifa zilizochapishwa na gazeti la Championi si za kweli, zinaharibu sifa nzuri ya Kaseja aliyojijengea kwa miaka mingi. Pia limemuweka katika mazingira magumu ya kuitumikia timu yake. Tunakusudia kulipeleka suala hili mbele ya sheria mapema wiki ijayo. Champion itabidi watoe ushahidi wa taarifa yao dhidi ya mteja wangu," alisema meneja huyo wa Juma Kaseja

Post a Comment

AddThis

 
Top