0


Tuliripoti kuhusiana na tukio lililotokea jijini Mwanza, ambapo mdogo wa msanii Dudu Baya "Mueta" alithibitisha kutokea kwa tukio la kukatwa skio kwa mama yao mkubwa ambae pia ni mama yake mkubwa na msanii Dudu Baya.

Habari hizo zilizothibitishwa na mdogo wake zinasema kuwa Dudu Baya ndio aliehusika katika tukio hilo la kumkata sikio mama yake mkubwa kwa madai kuwa anamloga  na kusababisha kutokufanikiwa kwa maswala yake
Dudu Baya nae azungumza upande wake


"kinachonishangaza kwenye hii ishu, polisi mwanza karibu wote wana namba zangu  za simu na hakuna kitu chochote nilichopigiwa, kwasababu mimi kama nina kesi polisi napigiwa tu simu bwana eeeh kuna tukio hili na hili tunakutaka saa flani na nnaenda sasa nashangaa sijapigiwa simu na sijui kama kuna kesi  kituo gani wala nini sasa hivi vitu wala sivielewi"

"mimi nawasiwasi hii inshu na ndugu zangu binafsi sawa, ndugu zangu nawajua vizuri hawa wa ukoo wangu na nilikuwa siwajui zamani wakati mi na-hit kwenye mziki labda mwaka 2000 nilikuwa nawapa ile priority ya juu kabisa lakini nilivyokuwa naenda mwanza kipindi cha nyuma ndugu zangu walikuwa wanaongea manenokibao, dudu baya hajajenga kwao kisesa hajafanya hivi, lakini mwisho wa siku nilisikitika san anilipoenda pale kisesa kujenga nyumba kwa ajili ya mama yangu mzazi self contained, four rooms, 

sasa nilishangaa ndugu zangu wamenuna wamekasirika hakuna hata wakuniambia big up wakati before walikuwa wanaongea maneno mengi.....kwa hiyo ni ndugu pia ambao ndio wana creat hili swala ili kunichafulia kwenye nionekana kwenye jamii namna gani.. lakini ninacho believe yule ni mama yangu mimi ni mwanae hivyo...."

Post a Comment

AddThis

 
Top