Algeria imeanza vizuri michuano ya Kombe la Mataifa Afrika kwa kuichapa Afrika Kusini kwa mabao 3-1.
Katika mechi hiyo ngumu katika mji wa Mongomo, Equatorial Guinea. Algeria ilitoka nyuma ikiwa nyuma kwa bao moja na kuibuka na ushindi huo wa mabao 3-1.
Kundi C ndiyo gumu zaidi na awali, Ghana ililala kwa mabao 2-1 dhidi ya Senegal.
Mechi hiyo hadi mapumziko ilikuwa sare ya bila bao, kabla ya mabao yote manne kufungwa katika kipindi cha pili.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Post a Comment