0
Michuano hiyo mwaka huu imekwama kufanyika kutokana na waliokuwa wamepangwa kuwa wenyeji, Ethiopia kujitoa na Katibu Mkuu wa Cecafa, Nicholas Musonye aliwaambia waandishi wa habari kwenye Uwanja wa Nyayo jijini Nairobi, Kenya juzi mabadiliko makubwa yatafanyika kuhusu michuano ijayo ya Kombe la Chalenji.
“Hatutakuwa na mashindano hayo mwaka huu lakini tunaangalia uwezekano wa kubadili mfumo mzima wa mashindano haya kuanzia mwaka ujao. Kamati ya Utendaji ya Cecafa itakutana tena wiki ijalo (wiki hii) na kutoa maamuzi ya mwisho ya namna mfumo mpya utakavyokuwa,” alisema Musonye.
Kuna uwezekano mkubwa michuano hiyo ikawa inachezwa nyumbani na ugenini kwa nchi za Ukanda wa Cecafa na zile zitakazokuwa zikialikwa kwa vile imeonekana kama ni gharama kubwa kuzikutanisha timu zote katika nchi moja.

Post a Comment

AddThis

 
Top