0
Wakati Shirikisho la Soka Uganda (FUFA) limetangaza kufuta mechi za kimataifa za kirafiki ambazo mabingwa watetezi wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara (VPL) walipanga kucheza dhidi ya timu tatu za Uganda nchini humo, kikosi cha Azam FC leo kimepoteza mechi yake ya kwanza dhidi ya SC Villa.
SC Villa, KCC FC na Vipers ni timu za Uganda ambazo Azam walipanga kucheza nazo nchini humo kujiandaa kwa mechi zinazofuata za VPL.
Baadhi ya mitandao ya michezo ya Uganda na Kenya imemkariri Msemaji wa FUFA Ahmed Hussein akieleza kuwa wamezipiga chini mechi za Azam FC nchini mwao kwa sababu hawajapata mawasiliano yoyote kutoka Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) juu ya ziara ya Azam FC nchini humo.
“Hatujapata taarifa yoyote rasmi kutoka TFF, kwa hiyo mechi zinazotarajiwa kuchezwa Uganda haziko katika ratiba yetu,” amesema msemaji huyo.
aza
Pia amesema waamuzi wa FUFA ambao walitarajiwa kuchezesha mechi hizo hawajataarifiwa kuhusu mechi hizo huku tamko hilo likiungwa mkono na pia na Sam Mpiima, Mkuu wa Kamati ya Waamuzi ya FUFA.
Hata hivyo, Azam FC leo jioni imepoteza mechi yake ya kwanza ziarani nchini humo ilipokubali kichapo cha mabao 3-2 dhidi ya SC Villa iliyomkuza mshambuliaji Mganda Emanuel Okwi wa Simba.
Azam FC ndiyo waliokuwa wa kwanza kuziona nyavu za wapinzani kwa bao la mshambuliaji Mrundi Didier Kavumbagu kabla ya mambo kugeuka kipindi cha pili na kujikuta wakiruhusu mabao mawili ya haraka kisha kuongezwa la tatu.

Post a Comment

AddThis

 
Top