0

Nimekuwa nikifatilia video nyingi zinazotengenezwa hapa BONGO kiukweli utakuta vituko vituko tu,japo wimbo mzuri lakini video huwezi hata kuangaliana wazazi wako

Eti wanaamini kukaa uchi ndiyo video inakuwa bora aua inapendwa sana kumbe siyo,,mimi naamini kizuri kinajiuza na kibaya kinajianika kwa stayle hizo ili kutafuta muonekano ambao mwisho wa siku malengo hayatimii

Kuna wamiliki na viongozi wa band za muziki hapa tanzania nilipata nafasi ya kukaa nao na kuzungumza mawili matatu kuhusu muziki wao,mafanikio na matatizo katika muziki na nilitakakujua kwanini band hizo zinashuka hazipati tuzo zile zinazoaminika ni kubwa hapa tanzania?

Majibu niliyatajia kuwa TUZO ZA KILL WANAPENDELEA kwa kigezo kuwa wao ni wakali na band inajaza hata ikienda mikoa mbali mbali watu wanajaa ukumbini

Ni kweli lakini kujaa kwa watu ukumbini sio kigezo ha wewe kupata Tuzo japo kwa nafasi chache ni moja ya kuonyesha band inakubalika

Kupata tuzo kuna mambo mengi yanazingatiwa hasa mavazi na ujumbe wa wimbo wenyewe ,ambapo haya ninayoyasema yanapatikana katika Video hii nzuri safi ya wimbo PESA ya ALONI JEANCY

Haikatazwi kuvaa viguo vya kubana lakini angalau maeneo fulani yasitiriwe ili kuwapa nafasi hata baba zenu wawapigie kura ili mpate tuzo

Aloni jeancy ni mwanamuziki mwenye asili ya congo na ni mwanamuziki wa muda mrefu hapa tanzania ambaye anaimba na band ya La Capital wazee sugu ya mzee wa heshima zake KING KIKI sambamba na clyton mpinga wazee wenye heshima na alama kwa taifa la tanzania kwenye upande wa burudani ..hilo halina ubishi

ALONI JEANCY AMEZINGATIA MAADILI YA KIAFRIKA KWA ASILIMIA MIA MOJA ,,



Post a Comment

AddThis

 
Top