0
Katika harakati yakutaka kutatua Mzozo ulioko kati ya Wanamuziki Inchini Congo,
Baada ya Onyo kali lililo tolewa na MEJA GENERALI KANYAMA CELESTIN, kuwataka Wanamuziki wajizuie na Mambo ya uchochezi , Nayule atakae endana kinyume cha Tamko hilo, Hatua kali ya Sheria Itachukuliwa dhidi yake.
Kufwatana na hayo, Majuzi kaitishwa kwa Haraka sana kwenye Makao makuu ya POLISI JIJINI KINSHASA MWANAMUZIKI MASHUHURI  » KOFFI OLOMIDE « ,kwatuhuma yakulitumia vibaya Jina la  » MZEE EBOLA  » kwa madhumuni yakuwatupia vijembe wenzie Wanamuziki. Jambo ambalo, MOPAO MOKONZI kalikanusha vikali kwakusema, Jina hilo la  » EBOLA « , wala hajajipa yeye bali kapachikwa kutoka kwa pande ya wapinzani wake.
Akiufwata mkondo wa GENERALI KANYAMA, MEA WA JIJI LA KINSHASA  » ANDRÉ KIMBUTA  » katoa msimamo wake nakupiga Marufuku  » WASEMAJI  » wa wanamuziki kwenye Vyombo vya habari. Tokea siku ya Leo , KAZI YA WASEMAJI WA WANAMUZIKI YAPIGWA MARUFUKU. Onyo hilo lawalenga pia  Vyombo Vya Habari, Haviruhusiwi kuwaalika kwenye vipindi vyao WASEMAJI wa wanamuziki. SHERIA KALI ITACHUKULIWA KWA WALE WATAKAO SHINDWA KUTEKELEZA AZIMIO HILO.
MEA ANDRE KIMBUTA, kasema Hali ya hewa ilikua Imeharibika kutokana na malumbano yasiokua na maana kati ya Wanamuziki Star Inchini CONGO, kwahiyo siku zijazo kawaalika WANAMUZIKI HAO KWENYE KIKAO KITAKACHO FANYIKA JIJINI KINSHASA, ILIKUJARIBU KUSAWAZISHA HALI YAUTATA ILIO JITOKEZA KATI YAO.
Wanamuziki wahusika kwenye Kikao hicho ni : KOFFI OLOMIDE, JB MPIANA, LE KARMAPA, NA FALLY IPUPA.

Post a Comment

AddThis

 
Top