Watoto wawili wa kiume wameishtaki Serikali na shirika la ndege la Malaysia kutokana na kumpoteza baba yao katika ndege ya Malaysia Airlines 370.
Watoto hao Jee Kinson mwenye miaka 13, na Jee Kinland wameorodhesha majina ya shirika hilo la ndege, maafisa wa idara ya usalama wa anga na uhamiaji, na mkuu wa kikosi cha jeshi la anga kuwa wamehusika moja kwa moja na upotevu wa ndege hiyo mwezi Machi 8 mwaka huu.
Baba wa watoto hao alikuwa mmoja wa abiria ndani ya ndege hiyo akitokea Kuala Lumpur Malaysia kuelekea Beijing China, tangu imepotea zimepita siku 237 na jitihada za kuitafuta bado zinaendelea.
Post a Comment