0


Brendan Rodgers akiwapa mbinu wachezaji wake kuelekea katika mchezo wa kundi B wa ligi ya mabingwa.

MSHINDI wa ligi ya mabingwa ulaya,Paul Scholes anaamini kuwa Liverpool wanaweza kutoa upinzani mkali katika mashindano ya mwaka huu.
Liverpool, mabingwa mara tano wa ulaya wamerudi tena katika michuano hiyo msimu huu baada ya kukosekana kwa miaka mitatu.
Majogoo hao wa jiji wanaanza kampeni yao leo jumanne kwa kuwakaribisha mabingwa wa Bulgaria, Ludogorets.
Pia watachuana na mabingwa watetezi Real Madrid na wakali wa Uswizi , Basle katika michezo ya kundi B.
Scholes aliyekuwepo katika kikosi cha Manchester United kilichotwaa ubingwa mwaka 2008, anatarajia kuona Anfield inakuwa sehemu ngumu kwa timu zitakazotua hapo.
Mkongwe huyo aliyasema hayo wakati akichambua ligi ya mabingwa katika kituo cha ITV.
Scholes alisema: “Liverpool ni farasi weusi katika michuano ya mwaka huu.
“Brendan Rodgers amefanya kazi kubwa. Staili ya uchezaji aliyochagua inavutia kuitazama na wachezaji wameonekana kumuelewa. Nahisi watafanya vizuri tena kwa aina ya wachezaji walionao”.
“Faida kubwa kwao ni mashabiki wa nyumbani. Anfield ni sehemu inayotisha kwenda wakati wote, kitu ambacho Manchester City wamekosa”


Kocha Brendan Rodgers
Liverpool walifanikiwa kufuzu UEFA baada ya kuonesha kiwango kikubwa msimu wa 2013/2014 wa ligi kuu England, lakini wakaishia kushika nafasi ya pili dhidi ya Manchester City.
Wamempoteza nyota wao Luis Suarez aliyejiunga na FC Barcelona, lakini Scholes anaamini Mario Balotelli anaweza kurithi nafasi hiyo.
Akimzungumzia Suarez, Scholes alisema: “Ni mchezaji mkubwa, lakini usisahau kuwa wamemsajili Balotelli, anaweza kuwa mshindi wa mechi pia”.

Post a Comment

AddThis

 
Top