0


KLABU za Simba na Yanga zimekaa kwa muda mrefu katika medani ya soka la Tanzania na kuwa kama ‘Tunu’ ya Taifa hili lenye mipango mibovu katika misingi ya uendeshaji wa mpira wa miguu.
Licha ya klabu hizi mbili kuwa na umri wa miaka zaidi ya 70 kwa sasa, bado hazijaweza kufanikiwa kwa ngazi ya kimataifa. Zimekuwa ‘Tia maji’ sana linapofika soka la ushindani.

Timu mpaka leo hazina hata viwanja vya mazoezi, hazina mfumo mzuri wa uuzaji wa jezi, hazina akademi wala kitu chochote cha maana.
Sio kwamba hazina wachezaji wazuri, mabenchi ya ufundi na rasilimali, hapana! . Matatizo yao ni mengi, lakini kubwa ni kwenye utawala.
Viongozi wao wengi wanaendesha mpira watakavyo wao, wanaendesha kwa mahaba bila kujali ueledi. Kifupi, siasa imetawala na watu wasiokuwa sahihi wanapewa mamlaka ya kufanya maamuzi ya kitaalamu klabuni.
Safari ndefu ya klabu hizi haijapata mafanikio mpaka tunapozungumza leo hii. Kwa bahati mbaya sana, klabu nyingine zinaiga siasa za Simba na Yanga.
Utawala mbovu unazitafuna klabu za Tanzania. Kwa mfano timu nyingi za majeshi zinalalamikiwa na makocha wengi .
Tatizo linaloelezwa sana ni viongozi wasiokuwa na utaalamu wa mpira kuingilia masuala ya kiufundi. Ni ajabu kuona katibu mkuu wa timu, ambaye hajui lolote kuhusu mpira, anaingilia kazi ya kocha. Anataka mchezaji fulani asajiliwe kwa matakwa yake, halafu mbaya zaidi analazimisha acheze.
Migogoro mingi baina ya makocha na viongozi inatokana na kuingiliana katika makujumu. Kocha anaweza kujikuta umepewa timu yenye wachezaji asiowataka, kuna soka hapo?
Kumekuwa na ladha ya mabadiliko katika soka la Tanzania hususani ngazi ya klabu, zimekuja timu zenye mapinduzi kama Mbeya City fc na Azam fc

Ngassa na Nyoni mambo yalipamba moto katika mchezo wa ngao ya jamii
Azam ni timu inayojadiliwa sana na imeaminiwa kuwa ina malengo ya kuleta mabadiliko ya soka la Tanzania kuanzia ngazi ya mabenchi ya ufundi, usajili wa wachezaji na utawala.
Hii ni timu iliyoanza vizuri na kuonekana kuendeshwa vizuri, lakini dhahiri kuna dosari za ndani sana ambazo si rahisi kuzijua.
Klabu inamilikiwa na watu wenye hela, na bahati nzuri wana nia ya dhati kuleta mapinduzi ya soka. Wametoa mabilioni ya fedha kujenga uwanja wa kisasa wenye vifaa vyote na wametoa mabilioni mengine kudhamini ligi kuu.
Hapa unaona kabisa wamiliki wa Azam fc wana nia ya kubadili soka la Tanzania na wanapenda sana klabu hii kuwa mfano. Wanataka iendeshwe kitaalamu na kufikia ngazi za juu.
Wamiliki wa Azam kila wanaloshauriwa ni wepesi kutekeleza, hawana longo-longo. Wakiambiwa mchezaji fulani anafaa, basi wanatoa hela za kumsajili.


Kocha mkuu wa Azam fc, Mcameroon, Joseph Marius Omog (kulia) akiwa na msaidizi wake Kalimangonga Ongala (kushoto)
Lakini tatizo lipo pale pale, wale watawala wanaoshauri mambo ya kiufundi, kweli wana ueledi wa soka? Jibu ni hapana!. Waliowengi hawana utaalamu wowote na wanajifanyia mambo kwa vile wamepewa nafasi tu.
Azam wana tatizo la kiutawala, hilo linajulikana na ndio chanzo cha kufanya vibaya na wasipochukua maamuzi magumu, basi watajikuta wanawekeza fedha nyingi, lakini wanaishia kushindana na Simba au Yanga.
Kiukweli, Azam sio klabu ya ngazi hizo, kwasababu imewekeza na kujijenga mno, hivyo inatakiwa kuwa na malengo ya mbali kama TP Mazembe.
Binafsi, nawalaumu baadhi ya viongozi wa Azam kwa kuliingilia benchi la ufundi na kulazimisha makocha wapange wachezaji fulani. Jambo kama hili limezitafuna kwa kiasi kikubwa Simba na Yanga.
Kuna watu ambao wana uhusiano na wamiliki wa Azam, hivyo wanatumia fursa hiyo kuingilia mipango ya benchi la ufundi wakati wao hawana utaalamu wala ufundi wowote wa mpira na hawajawahi kucheza hata ‘chandimu’ zaidi ya kusoma kwenye mtandao.
Watu hawa wanajifanya wanajua mpira, kumbe hawajui kabisa. Wanashinikiza wayapendayo wao na wamekuwa wakiwashauri vibaya wamiliki wa timu.

Mshambulaiji hatari wa Azam fc, Kipre Tchetche
Watu  wanatumia ufundi wa kuangalia mpira kwenye TV. Kwasababu tu wameona mpira unavyochezwa uwanjani, wametafakari kwa mawazo yao na kuchanganya ya kwenye mtandao, wanajiona kama wataalamu wa soka.
Mwisho wa siku wanatoa ushauri ‘bomu’ kabisa kwa wamiliki wa timu na wamejikuta kuwa mstari wa mbele kuiharibu Azam inayopewa heshima kubwa ya kubadili soka la nchi hii.
Watawala hawa wasiokuwa na ueledi, wamekuwa wakisajili wachezaji wao, wanatoa mapendekezo kwa wenye timu, wakitaka wachezaji gani wasajiliwe. Hatutaji majina, lakini itakapobidi tutawataja tu ili wajirekebishe na wawaachie walimu watoe mawazo yao.
Azam wasitake kushindana na Simba au Yanga,  kwasababu wao ni timu kubwa ambayo nchi nzima inaiangalia kama ndiye mkombozi wa soka la Tanzania.
Wao wanatakiwa kusimamia na kuendesha mambo yao kiueledi ili waonekane mfano wa kuigwa. Sasa hivi sio kwamba wana uwezo kuliko timu nyingine, bali kinachowabeba ni msuli wa hela.

Wana timu ambayo inamilikiwa na matajiri. Kwa bahati nzuri kila wanapoambiwa kitu wako radhi kutoa hela. Mfano mchezaji waliyemsajili kutoka Mali, Ismail Diarra ni kuwadanganya ‘mabosi’ tu, nadhani kuna kitu kingine katikati zaidi ya mpira.
Bahati mbaya zaidi watu hawa ni wachache tu, wanaleta mambo ya Kiswahili kama ya Simba na Yanga, wakati Azam wanatakiwa kuwa na mfumo wa kisasa.
Viwanda vya Bakhresa vinaendeshwa kwa kuajiri wataalamu kutoka India, Italia. Kuajiri wataalamu hawa kutoka nje ni ueledi.
Kama wanaweza kufanya hivyo kwa viwanda, basi na timu iwe vivyo hivyo, watafute wataalamu ili waiendeshe katika misingi ya taaluma kama kweli wanataka iwe taasisi inayojitegemea.
Sisi tunafanya kazi kubwa zaidi kuwekeza katika mabenchi ya ufundi, lakini tunasahau eneo lingine la upande wa utawala.
Kwa watu wanaotaka mabadiliko katika soka la Tanzania wanawategemea Azam fc, lakini kuna watu wachache wanaharibu mambo kwa kuendekeza maslahi binafsi na mahaba kwa baadhi ya mambo ya msingi.
Timu inaaminiwa na watu, inakwenda kucheza ligi ya mabingwa na timu kama TP Mazembe, Esperance na nyingine. Kinachotakiwa ni kujikita zaidi huko na sio kuangalia kuifunga Simba au Yanga. Kama wamefanikiwa kuchukua ubingwa, basi wajipange zaidi kwa ajili ya  ligi ya mabingwa.
Benchi la ufundi liko vizuri, lakini tatizo ni mambo ya utawala. Wakiweza kurekebisha hilo, Azam itakuwa mfano wa kuigwa.

Kwa mfano mambo ya rushwa yamekuwa yakijitokeza. Juzi walipofungwa na Yanga mabao 3-0 katika mchezo wa Ngao ya Jamii, kuna wachezaji wamekuwa wakilalamikiwa chini kwa chini. Azam fc wasitafute mchawi, mchawi ni wao wenyewe. Wamefungwa na Yanga kihalali.
Wanaanza sijui Sure boy, Kavumbagu, Mwadini wamechukua hela, sio kweli. Wanatakiwa kuacha kuwafanya wachezaji kama kivuli cha kukimbilia pale wanapofanya vibaya.
Ukitaka kujua kuwa viongozi ndio wenye matatizo, kumbuka lile sakata la akina Aggrey Morris, Erasto Nyoni, Said Mourad na kipa Deogratius Munish ‘Dida’.
Walisema wachezaji hawa wamehujumu mechi moj dhidi ya Simba sc. Wakaweka watu wa kuwachunguza na kupeleka kesi TAKUKURU, lakini hawakupatikana na kosa hilo na mpaka leo wamebaki kuwa wachezaji wa kutegemewa.
Wachezaji hawakuwa na tatizo, wenye tatizo ni viongozi. Kwahiyo kinachotakiwa kufanyika ni kujitathimini, kujitafakari, halafu kujiongeza.
Katika kujitafakari; wanatakiwa kukaa chini upya, kurejea mipango yao mama na kujikumbusha kuwa wana safari gani mbele yao.
Baada ya hapo wajitathimini ili wajue kama wamefanikiwa japo hata kidogo katika mipango yao na wajue mapungufu yako wapi.
Kama wanaona kuna matatizo wanatakiwa kujipanga upya. Cha msingi wabaini matatizo yako wapi na kuja kivingine.
Wakishajua matatizo yao, basi wajiongeze kwa maana ya kufanya maamuzi magumu hususani katika suala la utawala linaloonekana kuwa na matatizo.  Hapa wamelundikana watu wasiokuwa na ueledi na mpira na wanaaminiwa na wamiliki wa timu.
Hao ndio wachawi wa Azam fc. Kinachotakiwa ni kutafakari kwa kina suala la utawala, watathimini mapungufu yao na kukubali kutafuta watu wenye taalamu ya mpira hata kutoka nje.
Kama wamiliki watapata watu wenye taaluma katika utawala wa mpira na kuwekeza hela kama walivyofanya kwenye miundombinu, wachezaji na makocha, basi Azam itafika mbali.
Lakini kama wataendelea kuwakumbatia watu hawa wachache wasiokuwa na taaluma, basi timu itajikuta iko pale pale na itaishi miaka mingi kama Simba na Yanga bila kuwa na kitu cha kujivunia.
Tafakari! Chukua hatua! Nawatakiwa siku njema!.
 


 
Wana timu ambayo inamilikiwa na matajiri. Kwa bahati nzuri kila wanapoambiwa kitu wako radhi kutoa hela. Mfano mchezaji waliyemsajili kutoka Mali, Ismail Diarra ni kuwadanganya ‘mabosi’ tu, nadhani kuna kitu kingine katikati zaidi ya mpira.
Bahati mbaya zaidi watu hawa ni wachache tu, wanaleta mambo ya Kiswahili kama ya Simba na Yanga, wakati Azam wanatakiwa kuwa na mfumo wa kisasa.
Viwanda vya Bakhresa vinaendeshwa kwa kuajiri wataalamu kutoka India, Italia. Kuajiri wataalamu hawa kutoka nje ni ueledi.
Kama wanaweza kufanya hivyo kwa viwanda, basi na timu iwe vivyo hivyo, watafute wataalamu ili waiendeshe katika misingi ya taaluma kama kweli wanataka iwe taasisi inayojitegemea.
Sisi tunafanya kazi kubwa zaidi kuwekeza katika mabenchi ya ufundi, lakini tunasahau eneo lingine la upande wa utawala.
Kwa watu wanaotaka mabadiliko katika soka la Tanzania wanawategemea Azam fc, lakini kuna watu wachache wanaharibu mambo kwa kuendekeza maslahi binafsi na mahaba kwa baadhi ya mambo ya msingi.
Timu inaaminiwa na watu, inakwenda kucheza ligi ya mabingwa na timu kama TP Mazembe, Esperance na nyingine. Kinachotakiwa ni kujikita zaidi huko na sio kuangalia kuifunga Simba au Yanga. Kama wamefanikiwa kuchukua ubingwa, basi wajipange zaidi kwa ajili ya  ligi ya mabingwa.
Benchi la ufundi liko vizuri, lakini tatizo ni mambo ya utawala. Wakiweza kurekebisha hilo, Azam itakuwa mfano wa kuigwa.
- See more at: http://shaffihdauda.com/?p=6420#sthash.S69x1lsy.dpuf
 

Post a Comment

AddThis

 
Top