0
Sierra Leone ni miongoni mwa mataifa yanayopambana na mlipukio
Liberia imesimamisha shughuli zote za soka ikiwa ni jitihada ya kupambana na mlipuko wa virusi vya ugonjwa wa Ebola.

Kulikuwa na hatari ya maambukizi kwasababu mpira wa miguu ni mchezo wa kugusana, chama cha soka kilisema.

Idadi ya watu waliopoteza maisha kwa virusi hivyo Afrika Magharibi imefikia 672, kwa mujibu wa takwimu mpya za umaoja wa mataifa, UN.

Shiriki kubwa la usafiri wa anga ukanda wa Afrika Magharibi la Asky limesimamisha usafiri wa ndege kwenda miji mikuu ya Liberia na Sierra Leone kutokana na kuongezeka kwa hofu ya virusi hivyo.

Hilo ni shirika la pili kufikia maamuzi hayo kufuatia mlipuko wa Ebola.
Ebola imeua asilimia 90 ya watu waliopata ugongwa huo, lakini wagongwa wanaweza kupona kama wanapata matibabu ya mapema.
Ugonjwa huu unasambazwa kwa njia ya kugusana na mtu aliyeathirika.

Msisitizo mkubwa ni suala la usafi kwa watu.
Mlipuko huo kwa mara ya kwanza uliripotiwa nchini Guinea. Ukasambaa mpaka Liberia na Sierra Leone.

Wiki iliyopita, Nigeria, taifa lenye watu wengi zaidi Afrika, lilikumbwa na wasiwasi mkubwa wa kushambuliwa kutokana na  mfanyakazi wa serikali ya Liberia, Patrick Sawyer  kutua mjini Lagos kwa ndege ya shirikia la Asky.

Maofisi wote waliokutana moja kwa moja na Bwana Sawyer, mwenye miaka 40, wamekuwa katika uchunguzi na timu ya madaktari, wizara ya fedha ya Liberia ilisema.
Mr Sawyer alikuwa mfanyakazi wa wizara hiyo na alifariki dunia siku tano baada ya kuwasili mjini Lagos.

Mamlaka za Nigeria zimebaini watu 59 walikutana na Sawyer na wamewapimwa watu 20.
Ebola tangu mwaka 1976



Post a Comment

AddThis

 
Top