0

Fredy Felix Minziro alibebwa na mchezaji wake baada ya JKT Ruvu kuifunga Simba mabao 3-2 msimu uliopita ndani ya uwanja wa Taifa.

MAAFANDE wa JKT Ruvu Stars wametamba kufanya vizuri katika michuano ya ligi kuu soka Tanzania bara inayotarajia kuanza kushika kasi septemba 20 mwaka huu.

Kocha mkuu wa klabu hiyo, Fredy Felix Minziro ameuambia Mtandao huu  kuwa timu yao ilikuwa imeanza mazoezi na vijana au chipukizi na baadaye wakaanza na wa zamani.

Minziro aliongeza kuwa vijana hao wamewasajili kutoka katika mpango maalum wa kusaka vipaji ambao klabu iliuendesha kwa kualika vijana kutoka sehemu mbalimbali nchini kufanya majaribio klabuni hapo.

“Kwa ujumla suala la usajili limeenda vizuri kwa maana ya vijana wengi tuliowapa, kwa kiwango fulani wanaridhisha na ambao hawaridhishi tunawatoa. Naamini kwa vijana tunaowapa na kuwasajili tutakuwa na timu nzuri”.

“Nafahamu kuwa ligi itakuwa na ushindani mkubwa kutokana timu zilizopanda, lakini naamini vinaja tutakaowasajili watatusaidia. Nitafanya kazi ya ziada kwasababu timu yote ni mpya na baadhi ya wachezaji wa zamani tumewaondoa”.

Hata hivyo, Minziro alisema anahitaji kupata wachezaji wenye uzoefu katika kikosi chake, lakini wasiwe wengi zaidi kwasababu kuna wengine ameamua kuwabakisha.

“Ni kweli wachezaji wenye uzoefu wanahitajika, lakini wasiwe wengi, kwa maana ya kwamba uwachanganye na vijana. Kama nilivyokuambia, baadhi yao tumewapunguza, lakini wakonggwe nanaowataka inategemeana kidogo ni umri upi”.

Kocha mkuu wa JKT Ruvu, Fredy Felix Minziro ( wa kwanza kushoto) akiwa kazini msimu ulipita wa ligi kuu soka Tanzania bara

“Kama unavyojua wachezaji wengi wa JKT Ruvu wamekaa na timu kwa muda mrefu, kwahiyo wengine tumeamua kuwapumzisha na wengine tumewaacha ili tuwachanganye na damu changa”.

Tanzania haina mfumo sahihi wa soka la vijana, hivyo wachezaji wengi wanakosa misingi ya mpira, lakini Minziro alisema atajitahidi kuhakikisha anawajenga vizuri na watakuwa na kiwango cha juu.
“Ni kweli,  vijana wengi hawana misingi ya mpira kutoka chini, lakini ukiwa kama kocha lazima ufanye kazi ya zaida kwa maana ya kwamba,  yale mambo ambayo hawayaelewi, unaendelea kuyasisitiza na kuyafanyia kazi mpaka watakapokaa sawa. Kikubwa ambacho nakazania katika mazoezi yangu ni kuwaimarisha mwili na kuwapatia misingi ya mpira”. Alisema Minziro.

Pia kocha huyo amefurahishwa na kitendo cha shirikisho la soka Tanzania, TFF, kusogeza ligi kwa takribani mwezi mzima tangu tarehe ya awali iliyotangazwa ambayo ilikuwa Aosti 24 mwaka huu mpaka septemba 20.

“Kwangu mimi nimefurahishwa sana na TFF kusogeza ligi mbele, kwasababu unafahamu kwamba kuna wachezaji karibu 10 hawapo katika kikosi cha timu yangu. Wapo kwenye timu ile ya `kombaini` ya majeshi, sasa nilikuwa napata matatizo makubwa sana, timu ni mpya, halafu na wengine 10 hawapo, sasa utafanya mazoezi ya aina gani ndugu yangu?

“Kwahiyo kusogeza mbele,  nadhani itakuwa nzuri. Nadhani majeshi watamalrza mashindano yao Agosti 27, kwahiyo nitawapata vijana wangu na nitakuwa nao pamoja angalau kwa wiki mbili kabla ya kuanza ligi kuu”. Aliongeza Minziro.
 
Fredy Felix Minziro alibebwa na mchezaji wake baada ya JKT Ruvu kuifunga Simba mabao 3-2 msimu uliopita ndani ya uwanja wa Taifa.
Na Baraka Mpenja, Dar es salaam
MAAFANDE wa JKT Ruvu Stars wametamba kufanya vizuri katika michuano ya ligi kuu soka Tanzania bara inayotarajia kuanza kushika kasi septemba 20 mwaka huu.
Kocha mkuu wa klabu hiyo, Fredy Felix Minziro ameuambia Mtandao huu  kuwa timu yao ilikuwa imeanza mazoezi na vijana au chipukizi na baadaye wakaanza na wa zamani.
Minziro aliongeza kuwa vijana hao wamewasajili kutoka katika mpango maalum wa kusaka vipaji ambao klabu iliuendesha kwa kualika vijana kutoka sehemu mbalimbali nchini kufanya majaribio klabuni hapo.
“Kwa ujumla suala la usajili limeenda vizuri kwa maana ya vijana wengi tuliowapa, kwa kiwango fulani wanaridhisha na ambao hawaridhishi tunawatoa. Naamini kwa vijana tunaowapa na kuwasajili tutakuwa na timu nzuri”.
“Nafahamu kuwa ligi itakuwa na ushindani mkubwa kutokana timu zilizopanda, lakini naamini vinaja tutakaowasajili watatusaidia. Nitafanya kazi ya ziada kwasababu timu yote ni mpya na baadhi ya wachezaji wa zamani tumewaondoa”.
Hata hivyo, Minziro alisema anahitaji kupata wachezaji wenye uzoefu katika kikosi chake, lakini wasiwe wengi zaidi kwasababu kuna wengine ameamua kuwabakisha.
“Ni kweli wachezaji wenye uzoefu wanahitajika, lakini wasiwe wengi, kwa maana ya kwamba uwachanganye na vijana. Kama nilivyokuambia, baadhi yao tumewapunguza, lakini wakonggwe nanaowataka inategemeana kidogo ni umri upi”.
- See more at: http://shaffihdauda.com/?p=3402#sthash.tUWKJDUL.dpuf

Post a Comment

AddThis

Top