0


Nyumba ambayo ipo karibu na kambi ya fm academia alfajiri ya leo imewaka moto mkubwa na kuharibu mali zilizopo ndani ya nyumba hiyo

Nyumba hiyo ambayo eneo la mwananyamala imewaka moto mkubwa kiasi cha kuwatia hofu wanamuziki wa band ya fm academia ambao nyuba yao ipo jirani na nyumba 

Chanzo cha moto huo ni hitilafu ya umeme ambayo imepelelekea moto kuwaka na kusababisha hasara kubwa kwa wakazi waliyokuwa wakiishi katika nyumba hiyo na studio ya kurekodi 
Kwa mujibu wa mashuhuda waliyokuwa katika eneo la tukio waliiambia blog hii kuwa hakukuwa na mtu aliyekufa wala kujeruhiwa vibaya 
Juhudi za kumpata kamanda husika ili kujua kama kuna majeruhi na mauti hazikuweza kuzaa matunda


moto ukishika kasi huku wananchi wakijitahidi kuuzima
Wananchi wengine wakitazama kwa uchungu tukio ambalo limetokea





Blog hii inawaomba wanachi wote kwa ujumla kuzima vifaa vya umeme wakati ambapohavitumiki na vile ambavyo vinaonekana kuwa na hitilafu vibadilishwe haraka na kama kuna dalili ya shoti ya umeme toa taarifa kwa tanesco ili kupata msaada wa dharula




Post a Comment

AddThis

 
Top