Wakati ikidaiwa kuwa mwanadada Aunt Ezekiel anamzunguka Wema Sepetu na kula Penzi la shemeji yake Diamond, sasa ameamua kufunguka na kudai kuwa kamwe hawezi kumsaliti Wema na kikubwa anachokiheshimu ni kwamba anajua Diamond ni mpenzi wa ndugu yake....
. Aunt alisema hajawahi kulala na Diamond, wala kumuomba kutoka kimapenzi kama watu wanavyodhani bali wao ni marafiki wa karibu kwani anatambua kuwa Wema anampenda Diamond, na ndio maana wakati wote wanakuwa pamoja na si kwamba yeye ana lengo la kuchukua nafasi hiyo.....
"Mimi jamani sijawahi kutoka na Diamond na wala sina lengo hilo,najua yeye ni shemeji yangu kwa Wema,sasa inakuwaje na mimi nijipeleke wakati najua kinachoendelea?
"Hayo mambo siwezi kufanya na ninachohitaji kuwaambia mashabiki wangu ni kwamba kila mmoja ana mpenzi wake na hatuwezi kuibiana wanaume kama inavyodhaniwa," alisema Aunt.
Hata hivyo alisema kuwa safari zote wanazokuwa pamoja ni jibu tosha na kama angetaka kufanya hivyo ni wazi wangegombana na rafiki yake, kitu ambacho hataki kiwe hivyo.
Post a Comment