Timbwili la aina yake lilifumuka ndani ya gesti moja iliyopo Mbezi Afrikana jijini Dar es Salaam (jina kapuni), kufuatia kijana aliyefahamika kwa jina moja la Kelvin kumkuta chumbani mtu aliyedai ni mjomba wake, Joseph akiwa na mkewe wa ndoa, Emiliani.
Mkasa huo wa ajabu ulijiri usiku wa Jumamosi iliyopita kwenye gesti hiyo iliyopo Mbezi ya Afrikana jijini Dar es Salaam.
Mama mmoja aliyedai ni mpishi wa futari maeneo hayo, alipiga simu kwa mwandishi na kusema:
“Mimi ni mpishi wa futari hapa Mbezi Afrikana kuna baba mmoja na ndugu zake wanachakazana, kisa wamefumaniana kwenye gesti ya (akaitaja jina). Ipo hapahapa jirani njooni muwahi.”
Mwandishi bila kuzubaa alianza kuchukua picha za tukio hatua kwa hatua. Wakati Timbwili likiendelea, Joseph alikuwa akipiga mayowe kumuomba mpwa wake huyo amsamehe ili wayamalize kimyakimya na kumsihi asisambaze habari hizo zikafika mpaka nyumbani kwa mke wake.
Katika hali ya kushangza, wakati wawili hao wakiendelea kuangushana chumbani, mke huyo alipata upenyo na kuchoropoka, akatimua mbio kwa kuhofia kipigo na kukwepa kamera.
Timbwili la wajomba hao lilitulizwa na mlinzi wa gesti hiyo (jina halikujulikana) ambaye alitumia mabavu na kufanikiwa kuwadhibiti na kuwaweka kitako.
Baada ya kutulizwa, Kelvin aling’ang’ania waende polisi lakini mjomba mtu alikataa katakata akimbembeleza mpwa wake kwamba wayamalize na kuahidi kutorudia tena mchezo huo huku akisema mwanamke huyo alimuwekea mtego wa makusudi.
Kufuatia maombi ya watu, akiwemo mlinzi wa gesti hiyo, Kelvin alikubali kumsamehe mjomba wake ambaye naye ‘alijikomiti’ kimaandishi (kopi tunayo) kumlipa Kelvin fidia ya shilingi laki tano (500,000) na kuahidi kutorudia kummendea mke wake.
Post a Comment