Mtoto anaesoma madrasa katika msikiti wa Manyema Barabara ya saba Dodoma akiangali baadhi ya vitu vilivyoungua baada ya moto mkubwa kuzuka Msikitini hapo leo mchana.
Misahafu ya Dini ya kiislam ikiwa imekusanywa pamoja baada ya kuunguzwa na moto unaosadikiwa kusababishwa na shoti ya umeme ulionguza samani mbali mabali za msikiti wa manyema Dodoma.
Mkurugenzi wa manispaa ya Dodoma Robert Kitimbo kama wananchi wengine akitoka ndani ya msikiti wa manyema barabara ya saba alipoenda kushuhudia Madhara yaliyosababishwa na Shoti ya umeme baada ya moto mkubwa kulipuka msikitini hapo.
Moshi mkubwa ukitoka katika sehemu ya msikiti wa Manyema uliopo Barabara ya Saba Dodoma, amba po chanzo cha moto huo ni Hitilafu ya umeme.
Waumini wa Msikiti wa Manyema uliopo Barabara ya Saba Dodoma wakiangalia mabaki ya samani za msikiti huo ulioshika moto ambapo chanzo chake kinadaiwa kuwa hitilafu ya umeme.
Waumini wa Msikiti huo wakisukuma maji yaliyotumika kuzima moto uliokuwa umeshika katika msikiti huo baada ya Hitilafu ya umeme na kusababisha hasara kubwa.
wakitoa madhuria yanayotumiwa katika swala mbalimbali na waumini wa msitiki wa Manyema baada ya kuunguzwa na moto uliosababishwa na Hitilafu ya umeme
...................mwisho............
Post a Comment
Click to see the code!
To insert emoticon you must added at least one space before the code.