0

Wakati Roy Keane akiendelea kumzungumzia vibaya, usiku wa jana Sir Alex Ferguson jijini Dublin, Ireland kwa ajii ya shughuli ya kijamii.

Akiwa mgeni rasmi kwenye Dublin Chamber of Commerce, Fergie alipata nafasi ya kuongea na jamii na katika vitu vingi alivyoongea na alimzungumzia Roy Keane, akiwa kama mtu anayetaka kuumaliza ugomvi wao – Fergie alikaririwa akisema kwamba kwenye soka la hivi sasa wanakosekana watu kama nahodha wake wa zamani.

”Katika mika 15 iliyopita tumekuwa tukipata wachezaji ambao anakosa haiba wachezaji kama Bruces, the Robsons na Keanes.
Hii ilikuwa kwa sababu walikuzwa tofauti.”
Pia alizungumzia kuhusu msimu wa kihistoria wa United hasa fainali ya mabingwa wa ulaya 1999, pia akamtaja Keane kama kiungo bora barani ulaya  – pamoja na Paul Scholes.
”Tukio kubwa zaidi kwenye maisha yangu ya soka: Ilikuwa mwaka 1999 mjini FC Barcelona. Watu wengi wanasema tulipata bahati lakini ile ilitokana na ubora na hali ya kutaka kushinda ya timu iliyoshinda mechi hiyo. 
Hatukucheza vizuri katika kipindi cha kwanza hilo lazima niseme…. 
Nilikuwa na mapengo ya Roy Keane na Paul Scholes – viungo bora wawili barani ulaya.”

Post a Comment

AddThis

 
Top