0
AGUERO, MESSI, HIGUAIN, DI MARIA AKITOKEA KATIKATI……

Sergio Aguaro alicheza kwa kiwango cha chini katika kombe la dunia, majeraha yalitajwa kama sababu ya kuvurunda kwake. Alifunga mabao 16 katika ligi kuu ya England wakati akienda katika kombe la dunia, mshambulizi huyo wa mabingwa wa England, Manchester City tayari amefunga mabao matano msimu huu, anategemewa kuanza sambamba na Messi, na Gonzalo Higuain kama, kocha Martino ataichezesha timu yake katika mfumo wa 4-3-3.
Mchezaji bora wa Manchester United kwa sasa, kiungo-mshambuliaji, Angel Di Maria ataanza katika kikosi cha kwanza na anaweza kuwa ‘ mwiba mkali’ kwa safu mpya ya ulinzi ya Dunga. Di Maria alifunga mara moja na kupiga pasi tatu za mwisho wakati, Argentina ilipoichapa, Ujerumani kwa mabao 4-1, mwezi uliopita katika mchezo wa kimataifa wa kirafiki.

DUNGA ALIMTUMIA MIRANDA , BEIJING ANAMRUDISHA HAPO KUTHIBISHA UWEZO…
Miranda, mlinzi wa kati wa mabingwa wa Hispania, klabu ya Atletico Madrid ameitwa na Dunga. Licha ya kuwa katika kiwango cha juu kwa misimu mitatu sasa, mlinzi huyo ‘ amekwama’ kupata nafasi katika kikosi cha ‘ Wateule 11′, amekuwa akiitwa na wakati mwingine akiachwa kabisa, lakini ili kupata mafanikio atatikiwa kuhimarisha safu ya ulinzi ambayo iliruhusu mabao 13 katika michezo saba ya kombe la dunia, yakiwemo mabao 10 katika michezo ya nusu fainali na ule wa kutafuta mshindi wa tatu wa fainali hizo kubwa zaidi za soka duniani.

Miranda alicheza katika kikosi cha kwanza cha Brazil katika michuano ya Olimpiki, Beijing, 2008 anaweza kupangwa na nahodha, Thiago Silva na kukumbusha enzi wakati, Dunga akiandaa timu ya Brazil kwa ajili ya fainali za kombe la dunia, 2010 nchini, Afrika Kusini. Luiz Fillipe mlinzi wa pembeni wa Chelsea, kiungo wa PSG, Lucas Moura, pia ni baadhi ya machaguo yaliyokosekana katika kikosi cha ‘ Big Phiri’, Dunga amewaita si kwa maana ya kumkosoa kocha aliyepita, bali machaguo hayo yametazama viwango vya nyota hao kwa sasa.

Messi alifunga ‘ hat-trick’ wakati timu hizo zilipozalisha mabao saba katika mchezo wa kimataifa wa kirafiki, Juni 9, 2012. Argentina ilishinda kwa mabao 4-3. Mshambulizi Fred alifunga bao la kuongoza dakika ya 85, Novemba, 2012 na ilionekana kama bao hilo lingeipatia ubinngwa, Selecao lakini, Ignacio Scocco alisawzisha dakika ya mwisho ya mchezo katika uwanja wa Antonio Vespucio Liberti Ipira, Argentina. Dakika 90 za pambano la mwisho la ‘ Super clasico de las Americas zilimalizika kwa sare ya kufungana bao 1-1 na Brazil ikitwaa taji la pili kwa mikwaju ya penalti.

Post a Comment

AddThis

 
Top