0
MSUMBIJI INAWEZA KUFUZU AFCON , 2015, MOROCCO IKIENDELEA NA MWENDO HUU
Msumbiji imejiweka katika nafasi nzuri ya kuwania tiketi ya kufuzu kwa fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika ( AFCON) mwakani nchini, Morocco baada ya kuwasimamisha vinara wa kundi la Sita. Ikicheza katika uwanja wake wa nyumbani, Black Mambas walipata bao la kuongoza katika dakika ya mwisho ya kipindi cha kwanza kupitia kwa mshambulizi, Kito.

Cape Verde ambao walishinda michezo miwili iliyopita dhidi ya Niger na Zambia, ilimalizwa na bao la kiungo mshambulizi, Reginaldo katika dakika ya 66. Mchezo mwingine wa kundi hilo ulikuwa sare ya bila kufungana hadi mapumziko, kati ya wenyeji Niger na mabingwa wa mwaka 2o12, Zambia. Baada ya matokeo hayo Msumbiji insshika nafasi ya pili ikiwa na pointi tano, pointi moja nyuma ya Cape Verde wanaoongoza kundi. Zambia na Niger zilikuwa na pointi mbili kila mmoja kabla ya mchezo wa usiku huu.
UGANDA YACHAPWA NA TOGO, KAMPALA

Togo imefufua matumaini ya kufuzu fainali za mwakani za Mataifa ya Afrika baada ya kuchomoza na ushindi ‘ mwembamba’ jijini, Kampala baada ya kuwalaza wenyeji Uganda kwa bao 1-0. Uganda ambao wa walilazimisha sare na Ghana ugenini kisha kuichapa Guine kwa mabao 2-0 imepoteza mchezo wa kwanza katika ardhi ya nyumbani baada ya miaka zaidi ya kumi.
Bao la dakika ya 30 lilidumu hadi filimbi ya mwisho na kuwapatia Togo ushindi wa kwanza baada ya kufungwa na Guinea na Ghana katika michezo miwili ya awali. Katika kundi la Tano. Ghana wanaongoza kundi hilo kutokana na wastani mzuri wa mabao ya kufunga na kufungwa, licha ya kulingana pointi na Uganda.

Ghana itakuwa na nafasi ya kuongeza pengo la pointi na kufikia mbili kama wataifungga Guinnea ugenini usiku huu. Guinnea wana nafasi pia ya kuongoza kundi hilo kama wataichapa timu hiyo ya kocha Akwesi Appiah. Guinnea wamepata ushindi mara moja dhidi ya Togo na wana pointi tatu katika michezo miwili iliyopita.

IVORY COAST YAPATA USHINDI WA PILI, CAMEROON YABANWA
Wilfried Bony alifunga bao la kuongoza kwa timu yake ya Taifa ya Ivory Coast katika dakika ya 25. Bao ambalo lilidumu hadi nusu ya kwanza ilipomalizika Cedric Mongongo aliisawazishia Congo DR kwa mkwaju wa penalti katika dakika ya 68. Wakati hali ilikuwa ‘ tete’ kwa timu hiyo ya Afrika Magharibi, mchezaji, Max – Alain Gradel aliwafungia ‘ Tembo’ bao la ushindi katika dakika ya 84 na kuwapatia ushindi wa Pili katika kundi la Nne

Vinara wa kundi hilo, Cameroon walilazimisha suluhu-tasa ugenini dhidi ya Sierra Leone na kuendelea kuongoza kundi hilo kwa pointi moja zaidi ya ‘ Tembo’ DRC imebaki katika nafasi ya tatu ikiwa na pointi zake Tatu baada ya kucheza michezo mitatu huku Sierra Leone wakivuta mkia baada ya kukusanya pointi moja katika michezo mitatu waliyocheza.

MALAWI, ETHIOPIA ‘ ZAPIGWA’ NYUMBANI ZIKIWA ‘ TAABANI’ KUNDI LA PILI
Ni kama nafasi za kufuzu kutoka kundi la Pili zitakwenda kwa nchi za Algeria Mali kufuiatia nchi hizo za Kakazini na Magharibi mwa Afrika kuchomoza na ushindi katika michezo yao ya leo.Algeria ilishinda Rafik Halliche na Djamer Mesbah kila mmoja alifunga kila kipindi na kuwasaidia ‘ mbwa mwitu wa Jangwani’ kuchomoza na ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Malawi wakicheza ugenini.

Huko, Adid Ababa, Ethiopia wenyeji walichapwa mabao 2-0 na Mali. Abdoulaye Diaby alifung a bao la kuongoza kwa wageni katika dakika ya 33, nusu saa kabla ya mchezo kumalizika, Sambou Yatabare aliwakikishia Mali ushindi wa pili katika kundi hivyo kujiweka nyuma ya Algeria kwa tofauti ya pointi tatu. Malawi wanashika nafasi ya tatu wakiwa na pointi tatu huku Ethiopia wakiburuza mkia pasipokuwa na pointi yoyote.

‘ BAFANA BAFANA’ INARUDI KWA KASI , YASHINDA UGENINI
Ilikuwa ni lazima Afrika Kusini waishinde timu ngumu ya Congo Brazaville kama wanahitaji kucheza fainali za AFCON mwakani nchini Morocco. Ikicheza ugenini, Bongani Ndulula aliifungia ‘ Bafana Bafana- Wavulana’ bao la kuongoza katika dakika ya 52, Tekelo Rantie akaongeza lingine dakika mbili baaae na kuisaidia timu hiyo kuchomoza na ushindi wa mabao 2-0 na kujikita kileleni mwa kundi la kwanza wakiwa na pointi saba.

Nigeria, wapo uwanjani kucheza na Sudan Kaskazini, jijini, Khartoun wapo nyuma ya Congo Braaville kwa tofauti ya pointi nne, ila watahitajika kufanya kila kitu ili kufufua matumaini ya kupata tiketi ya kutetea ubingwa wao. Wakiwa na pointi mbili katika nafasi ya tatu, kikosi cha ‘ Kocha mzalendo’ Stephen Keshi kitatakiwa kufuta historia mbaya Sudan ili kujivuta katika msimamo.

Post a Comment

AddThis

 
Top