0
Kocha Mkuu wa Simba, Patrick Phiri amewaambia wachezaji wake kuwa kuna kitu amekiona baada ya sare dhidi ya Orlando Pirates ya Afrika Kusini.


Simba imetoka sare ya bila kufungana dhidi ya Orlando Pirates katika mechi ya kirafiki iliyochezwa leo jijini Johannesburg.
Simba iliwakosa wachezaji wake walio kwenye kikosi cha Taifa Stars pia Emmanuel Okwi ambaye ameitumikia Uganda, leo.

Phiri raia wa Zambia, amewaambia wachezaji wake kuwa moja ya kitu alichokiona ni hali ya kujiamini kurejea.
“Kocha amefurahishwa na tulivyocheza, ingawa tulicheza na timu kubwa, lakini tulionyesha kujiamini.
“Orlando walichanganya na wachezaji kadhaawa timu ya vijana kwa kuwa wachezaji wao wengine walikuwa wamekwenda kuitumikia timu yao ya taifa kwenye michuano ya kuwania kuchea Kombe la Mtaifa Afrika,” kilieleza chanzo.
“Lakini mechi ilikuwa ngumu sana, jamaa wako fiti lakini tuliwadhibiti vizuri kabisa.
“Hata baada ya mchezo nao walifurahia na kusema ilikuwa ni mechi nzuri na itakayowasaidia.”
Phiri amewasisitiza wachezaji wake kuendelea kujiongeza kutoka walipo na kwenda mbele kwa mafanikio zaidi.

Simba imeamua kwenda kuweka kambi nchini Afrika Kusini kutokana na mambo mawili, kuanza kwa sare tatu mfululizo lakini kujiandaa dhidi ya Yanga Oktoba 18.

Post a Comment

AddThis

 
Top