Taarifa kuhusiana na mastaa mbali mbali ikiwemo wa muziki, filamu, na michezo kuingia katika headline zinazowangumzia kujihusisha na siasa sio taarifa ngeni kuzisikia, ambapo kwa sasa mastaa wa movie wanaingia kwenye headline nyingine ya wao kwa wao kugombea nafasi ya ubunge kwenye jimbo moja kupitia vyama tofauti.
Mastaa wa filamu kutoka Nigeria Bob Manuel Udokwu na Tony One Week Muonago wanaendelea kuzungumziwa sio kwa sababu wamejiingiza kwenye siasa, bali kinachozungumziwa ni kitendo cha wao kugombea nafasi hiyo katika jimbo moja kitu ambacho kimeanza kuvutia hisia za watu wengi.
Bob Manuel Udokwu anagombea kupitia chama cha APGA na Tony One Week Muonagor anagombea kwa tiketi ya ACN katika jimbo moja la Anambra, Nigeria ambapo uchaguzi mkuu wa nchi hiyo unatarajiwa kufanyika katikati ya mwaka 2015, ambapo staa mwingine wa Nollywood ambaye alitangaza kujiingiza kugombea ubunge ni Desmond Elliot.
Post a Comment