Pamoja na mateso hayo, staa huyo wa filamu alisema anafurahia maisha yake kama mtu maarufu ikiwamo na kuandikwa na vyombo vya habari mara kwa mara.
“Kuna wakati najutia kuwa maarufu kwa asilimia kama 40 hivi lakini nashukuru kwani kwa asilimia 60 nayafurahia maisha yangu.
“Ukiwa nyota kuna changamoto nyingi sana, kuna wakati mtu anaweza kukuandika habari inayokufanya ushindwe hata kutoka nje na kubaki ndani tu,”alisema.
Wema alisema kuna wakati huwa anatamani asingekuwa maarufu kwani akifanya kitu kidogo hata kama ni cha kawaida lakini hupokelewa kama habari kubwa na kuongelewa sana.
“Lakini katika maisha kama haya sina cha kufanya japo kuna mambo ambayo huniumiza na najitahidi sana kuvumilia,” alisema.
Post a Comment