0

Mlinzi, Giorgio Chiellini alifunga mara tatu na kuisaidia Italia kushinda mchezo wa pili mfululizo kuwania tiketi ya kufuzu kwa fainali za Ulaya, Euro, 2016, Ufaransa. Italia walikuwa katika kipindi kibaya, wakipoteza nafasi kadhaa za kufunga mabao kabla ya bao la kichwa la mlinzi huyo wa klabu ya Juventus. Chiellini alifunga bao hilo katika dakika ya 44 kuelekea mwisho wa kipindi cha kwanza.

Mchezaji huyo alifunga bao la pili katika dakika ya 77 lakini hili lilikuwa langoni kwa kipa wake, Gig Buffon. Aliisaidia Azerbaijan kusawazisha lakini alirudi kwa kasi na kufunga bao la ushindi zikiwa zimesalia dakika tisa mpira kumalizika. Italia iliifunga Norway katika mchezo wa kwanza ikicheza ugenini, imefanikiwa kushinda mchezo wa pili mfululizo sambamba na Jamhuri ya Czech ambao waliifunga Uturuki kwa mabao 2-1 katika uwanja wa Atuturk Olympic Stadium, Uturuki

Post a Comment

AddThis

 
Top