0
Ikicheza katika uwanja wa nyumbani, Amsterdam Arena, timu ya Taifa ya Uholanzi ‘ ilishtushwa’ na bao la uongozi kutoka kwa wageni, Kazakhstan kupitia kwa mchezaji, Renat Abdulin dakika ya 18. Ikiwa na mastaa kama, Wesley Sneijer, Arjen Robben, Ibrahim Afellay, Nigel De Jong na nahodha, Robbin Van Persie kikosi cha Guus Hiddink kilihitaji msaada kutoka kwa ‘ super-sub’ Klans Jan Huntelaar, dakika ya 62, Afellay dakika ya 82 akafunga bao la pili, kisha Van Persie akafunga bao la tatu kwa mkwaju wa penalti katika dakika ya 89.

Huo ni ushindi wa kwanza kwa Uholanzi katika harakati za kufuzu kwa fainali za Ufaransa, 2016 baada ya kupoteza mchezo wa kwanza dhidi ya Jamhuri ya Czech. Hiddink kocha ambaye amechukua nafasi ya Luis Van Gaal alijiunga na Manchester United mara baada ya kumalizika kwa kombe la dunia amepata ushindi wa kwanza baada ya kufungwa na Italia mwezi uliopita kwa mabao 2-0.

Post a Comment

AddThis

 
Top